Wanawake TBL Group wajiunga na programu ya mwanamke wa wakati ujao ya ATE | LUKAZA BLOG

Wanawake TBL Group wajiunga na programu ya mwanamke wa wakati ujao ya ATE

Wanawake watatu kutoka kampuni ya TBL Group wamechaguliwa kujiunga na mpango wa mwanamke wa wakati ujao ambao imeanzishwa na Chama Cha Waaj...

Wanawake watatu kutoka kampuni ya TBL Group wamechaguliwa kujiunga na mpango wa mwanamke wa wakati ujao ambao imeanzishwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa kushirikiana na Shirikisho la Vyama vya Waajiri nchini Norway ambao umeenga kuboresha ufanisi wa wafanyakazi wa kike mahali pa kazi hapa nchini.
Mpango huu ambao umezinduliwa jijini Dar es Salaam unawashirikisha wanawake wapatao 33 kutoka makampuni mbalimbali nchini ambao watapatiwa mafunzo mbalimbali ya uongozi.
Akiongea kwa niaba ya wenzake Meneja wa kuendeleza vipaji wa TBL Group Lilian Makau Galinoma ambaye amechaguliwa kushiriki katika mpango huu alisema  wanashukuru kampuni yao kwa kuona umuhimu wa kuendeleza wafanyakazi wake.
“Tunaishukuru kampuni yetu kwa kutufadhili ili tuweze kupata mafunzo ya uongozi na tuna imani yatatupa upeo zaidi wa kuboresha utendaji wa kazi zetu za kila siku ikiwemo kuendeleza vipaji vya wafanyakazi wenzetu wa  kike  “.Alisema.
 Meneja wa kuendeleza  Vipaji wa TBL Group Lilian Makau Galinoma akitoa mada wakati wa uzinduzi wa mpango wa    Mwanamke wa wakati  ujao Tanzania ( Female Future Tanzania) ulioanzishwa na  na Chama Cha waajiri Tanzania( ATE) .Uzinduzi ulifanyika katika iliyofanyika hoteli ya Sea Cliff   jijini Dar es Salaam
 Mkurugenzi Mkuu  wa Chama cha Waajiri Tanzania ( ATE) Dk.Aggrey Mlimuka (kulia) akimpongeza  Meneja wa kuendeleza  Vipaji wa TBL Group  Lilian Makau Galinoma mara baada ya kumaliza kutoa mada wakati wa uzinduzi wa Progamu ya   Mwanamke wa wakati ujao Tanzania ( Female Future Tanzania) iliyoandaliwa na Chama cha waajili Tanzania( ATE) katika  hoteli ya Sea Cliff   jijini Dar es Salaam
 Watendaji waandamizi wa taasisi mbalimbali wakiwa katika picha ya washiriki wa mpango wa   Mwanamke wa wakati  ujao Tanzania ( Female Future Tanzania) wakati wa uzinduzi wake katika hoteli ya  Sea Cliff   jijini Dar es Salaam
 Mkurugenzi Mkuu  wa Chama cha Waajiri Tanzania ( ATE) Dk.Aggrey Mlimuka (wa pili kulia ) akibadilishana mawazo na  Meneja  Vipaji wa TBL Group  Lilian Makau Galinoma (wa pili kushoto)  wakati wa  uzinduzi wa mpango wa   Mwanamke wa Wakati  Ujao Tanzania ( Female Future Tanzania) utakaoendeshwa  na Chama cha waajiri Tanzania( ATE) .Kushoto ni Meneja bidhaa wa Kiwanda cha  Konyagi (DTL)Warda  Kimaro na Meneja Mkuu  mpishi wa pombe wa  Chibuku.(DARBREW) Neema Arora. Uzinduzi umefanyikakatika  hoteli ya Sea Cliff   jijini Dar es Salaam
 Mkurugenzi Mkuu  wa Chama cha Waajiri Tanzania ( ATE) Dk.Aggrey Mlimuka (wapili kulia ) akisalimiana na  Meneja  Vipaji wa TBL Group  Lilian Makau Galinoma (wapili kushoto)  wakati wa Warsha ya   Mwanamke wa Wakati  Ujao Tanzania ( Female Future Tanzania) ulioandaliwa na Chama cha waajiri Tanzania( ATE)  katika  haoteli ya Sea Cliff  jijini Dar es Salaam, leo.Kushoto ni Meneja bidhaa wa Kiwa nda cha  Konyagi (DTL) na Meneja  Mkuu  mpisha wa pombe wa  Chibuku.(DARBREW) Neema Arora.
Baadhi ya washirki wa Warsha ya Mwanamke wa Wakati Ujao Tanzania ( FEMALE FUTURE TANZANIA) wakimsikiliza  mada mbalimbali zilizotolewa wakati wa uzinduzi wake  katika  haoteli ya Sea Cliff   jijini Dar es Salaam

Related

kitaifa 7576448966831828558

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item