Bila Maji Hakuna Uhai’ ya TBL Group yaleta faraja kwa jamii | LUKAZA BLOG

Bila Maji Hakuna Uhai’ ya TBL Group yaleta faraja kwa jamii

Diwani wa kata ya Mchikichini wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Joseph Ngowa,ameishukuru kampuni ya TBL Group kwa jitihada zake za kusa...

Diwani wa kata ya Mchikichini wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Joseph Ngowa,ameishukuru kampuni ya TBL Group kwa jitihada zake za kusaidia kuwapatia maji safi wakazi wa maeneo yaliyopo jirani na viwanda vyake na kuzingatia kanuni za utunzaji wa mazingira.
 
Bw. Ngowa aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati Mkurugenzi wa Masuala ya Nje wa kampuni ya SABMiller kanda ya Afrika,Bw.Monwabisi Fendeso,alipotembelea moja ya mradi wa maji kwa jamii unaofadhiliwa na TBL Group wilayani Ilala kupitia mradi wake wa kuwezesha jamii kupata maji safi unaojulikana kama ‘Bila Maji Hakuna Uhai’.
 Bw.Monwabisi Fendeso (Katikati) akipatiwa maelezo na viongozi wa kata ya Mchikichini,wilayani Ilala
Bw.Monwabisi Fendeso (Katikati) akinawa maji alipotembelea mradi wa maji wa TBL jijini Dar es Salaam wengine pichani ni viongozi wa kata ya Mchikichini,wilayani Ilala

Kwa upande wake,Fendeso, alisema kuwa  kampuni ya SABMiller kupitia kampuni yake  tanzu ya TBL Group itaendelea kuunga mkono jitihada za serikali katika kutekeleza miradi ya kuwapatia wananchi maji safi ,utunzaji wa mazingira,kuwezesha akina mama kiuchumi na kutoa elimu ya biashara kwa wajasiriamali nchini na utekelezaji wa baadhi ya miradi hiyo unaendelea vizuri.
 

Kampuni ya SABMiller ambayo ni kampuni mama ya kampuni ya TBL Group tayari imeanza kutekeleza programu mbalimbali za kuinua sekta ya viwanda na kilimo nchini ikiwemo programu ya Go Farming ya kuendesha kilimo shirikishi na wakulima ambayo tayari imenufaisha wakulima wa zao la Shahiri kanda ya Kaskazini mwa Tanzania na wakulima wa zabibu mkoani Dodoma.

Related

Hot Stories 6777496447906104899

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item