Bintiye Obama afanya kazi mgahawani | LUKAZA BLOG

Bintiye Obama afanya kazi mgahawani

Image copyright AP Image caption Sasha Obama, 15, akifanya kazi Sasha Obama, bintiye Rais wa Marekani Barack Obama, ameamua kuacha '...

Sasha Obama, 15, akifanya kazi

Image copyrightAP
Image captionSasha Obama, 15, akifanya kazi
Sasha Obama, bintiye Rais wa Marekani Barack Obama, ameamua kuacha 'starehe' za ikulu ya White House na kuanza kufanya kazi katika mgahawa mmoja, vyombo vya habari nchini Marekani vinaripoti.
Binti huyo wa umri wa miaka 15 ameanza kufanya kazi ya kuwahudumia wateja katika mgahawa mmoja ulioko Martha's Vineyard, Massachusetts.
Sasha, ambaye anatumia jina lake kamili, Natasha, aliandamana na maafisa sita wa ulinzi wa secret service siku yake ya kwanza kazini, gazeti la Boston Herald linaripoti.
Familia ya Obama hutembelea eneo hilo sana wakati wa likizo.
Picha zinazosambazwa zinamuonesha bintiye huyo mdogo wa Obama akiwa amevalia sare ya hoteli akifanya kazi.
Mfanyakazi mmoja katika mgahawa huo aliambia gazeti hilo la Herald: "Tulikuwa tunashangaa ni kwa nini kulikuwa na watu sita walikuwa wanamsaidia msichana huyu, lakini baadaye tukagundua alikuwa nani."bbc swahili

Related

Kimataifa 6641962038394392286

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item