MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU AHUDHURIA UFUNGUZI WA MKUTANO WA 36 WA SADC MJINI MBABANE SWAZILAND | LUKAZA BLOG

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU AHUDHURIA UFUNGUZI WA MKUTANO WA 36 WA SADC MJINI MBABANE SWAZILAND

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) akiwa kwenye mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Se...

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) akiwa kwenye mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) uliofunguliwa leo kwenye ukumbi wa Mandvulo uliopo Lozitha, Swaziland.
 Mfalme Mswati wa III (kushoto) akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC kwenye ukumbi wa Mandvulo, Lozitha Swaziland.
 Binti akionyesha bendera ya Tanzania wakati wa kuimba shairi maalum ya ufunguzi wa mkutano wa 36 wa SADC
 Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa 36, Lozitha Swaziland.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini ubao wa kumbukumbu kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli wenye majina ya viongozi waliohudhuria mkutano wa 36 wa SADC uliofanyika Lozitha, Mbabane Swaziland.


Mwenyekiti anayemaliza muda wake wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika -SADC- ambaye pia ni Rais wa  Botswana Luteni Jenerali Dkt. Seretse Khama Ian Khama amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kwake kwa kishindo katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana.Rais huyo wa Botswana ametoa kauli hiyo ya pongezi katika hotuba yake 
kwenye ufunguzi wa Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC
unaofanyika Mbabane- Swaziland ambapo Katika Mkutano huo Rais wa Jamhuri ya 
Muungano wa Tanzania Dakta JOHN POMBE MAGUFULI anawakilishwa Makamu wa Rais wa 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. 
Rais huyo wa Botswana amesema ukuaji wa demokrasia katika nchi wanachama wa jumuiya ya SADC unaendelea kuimarika hivyo ni muhimu jitihada hizo zikaendelezwa zaidi.


Amesema ana Imani  kubwa na Viongozi waliochaguliwa kwa njia ya
amani,uhuru  na haki katika ukanda wa SADC akiwemo Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na Rais wa Jamhuri ya Visiwa shelisheli kwamba watafanya 
kazi kwa bidii ili kuharakisha maendeleo kwa wananchi wao.

Wakuu wa nchi na Serikali wa SADC katika mkutano huo wameshuhudia utoaji 
wa zawadi mbalimbali kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika utunzi wa insha na 
kwa wanahabari ambao wameandika habari mbalimbali kuhusu SADC ikiwemo masuala 
ya huduma ya maji.

Aidha Katika Mkutano huo wa 36 wa SADC viongozi 
wanaohudhuria watafanya uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa SADC na
Uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Siasa, Ulinzi 
na Usalama ( SADC Troika)

Katika mkutano huo Wakuu wa nchi na serikali pia watapokea rasimu za
maboresho ya mikataba mbalimbali kutoka kwenye Baraza la Mawaziri kwa ajili ya 
kutia saini. Miongoni mwa rasimu hizo ni mkataba wa kuboresha itifaki ya SADC 
dhidi ya rushwa, maboresho ya itifaki ya ushirikiano wa siasa, ulinzi na 
usalama ya SADC na maboresho ya itifaki ya biashara.

Related

kitaifa 7166501297505948068

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item