MCHUNGAJI DKT.DANIEL KULOLA WA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA MWANZA KUITETEMESHA INJILI KWA MARA NYINGINE NCHINI MAREKANI. | LUKAZA BLOG

MCHUNGAJI DKT.DANIEL KULOLA WA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA MWANZA KUITETEMESHA INJILI KWA MARA NYINGINE NCHINI MAREKANI.

Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya la Jijini Mwanza, akihubiri katika moja ya mikutano yake iliyofanyika mkoani Morogoro. Kwa...

Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya la Jijini Mwanza, akihubiri katika moja ya mikutano yake iliyofanyika mkoani Morogoro.

Kwa mara nyingine Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza, Dkt.Daniel Moses Kulola, amepata kibali cha kupeleka neno la Mungu katika bara la Amerika.

Itakumbukwa kwamba ni miezi michache tu baada ya kupata kibali kama hicho ambapo alihubiri katika majimbo ya Dallas, Houston, Fortworth, Boston, Connectcut, Ohio Cincinnati na New York nchini Marekani.

Pia Dkt.Kulola, alipata kibali cha kuhudumu nchini Canada katika Kanisa kubwa la The Global Kingdom pamoja na miji mbalimbali kama vile Ottawa, Quebec na Toronto.


"Watu wengi walibarikiwa na kuinuliwa kimwili na kiroho kwani injili yangu ni kuyashughulikia maisha ya watu kiroho na
kimwili". Anasema Dkt.Kulola ambaye awamu hii amepata kibali cha kuhudumu katika miji ya Boston, Dallas na Arizona nchini Marekani.


"Nataraji Bwana atatenda mambo makubwa huko, ninaomba maombi yenu kwa nguvu zote". Anadokeza Dkt.Kulola na kuwasihili watakaohitaji kuwasiliana nae watumie nambari za simu +255 767 749 040 kwa Tanzania na +1 832 777 5032 kwa Marekani.

Huduma za Mchungaji Dkt.Kulola zinatarajia kuanza agost 09,2016 nchini Marekani na kufikia tamati Agost 25,2016 ambapo safari ya kurejea Tanzania itakua imewadia.
Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya la Jijini Mwanza, akihubiri katika moja ya mikutano yake iliyofanyika barani Amerika.

Related

Kimataifa 7679107317387063122

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item