MFUKO KICHOCHEO WA SAGCOT WASAINI MAKUBALIANO NA SHIRIKA LA BOTHAR KUTOKA NCHINI IRELAND | LUKAZA BLOG

MFUKO KICHOCHEO WA SAGCOT WASAINI MAKUBALIANO NA SHIRIKA LA BOTHAR KUTOKA NCHINI IRELAND

Katibu Mtendaji wa Mfuko Kichocheo wa SAGCO Bwa. John J. Kyaruzi akisaini makubaliano hayo na Mwasisi wa Shirika la Bothar Bwa. Peter Ireto...


Katibu Mtendaji wa Mfuko Kichocheo wa SAGCO Bwa. John J. Kyaruzi akisaini makubaliano hayo na Mwasisi wa Shirika la Bothar Bwa. Peter Ireton huku wakishuhudiwa na Dkt. Bernard Muyeya (kulia) Mkurugenzi wa Huduma za Nje ya Nchi wa Bothar na Bwa. Abdallah S. Msambachi ( kushoto) Mratibu wa Biashara wa Mfuko wa SAGCOT. 
Ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa kuongeza tija na uzalishaji kwa
wafugaji wa ng’ombe wa maziwa mkoani Njombe, Iringa na Mbeya, Mfuko
Kichocheo wa SAGCOT yaani SAGCOT CATALYTIC TRUST FUND tarehe 12 Agosti 2016 umesaini makubaliano na Shirika la Bothar kutoka nchini Ireland ambalo linajihusisha na kutoa misaada mbalimbali inayolenga kutoa fursa kwa familia zenye kipato cha chini kuweza kuboresha maisha yao kupitia uwekezaji wa shughuli zinazowaletea kipato hususani kaya
zinazojishughulisha na ufugaji.

Katika makubaliano hayo jumla ya Ng’ombe wa kisasa 630 wanatarajiwa kuingizwa nchini katika kipindi cha miaka mitatu. Ng’ombe hao watagawiwa kwa wafugaji walioandaliwa chini yamiradi inayotekelezwa na Mfuko huo, Aidha wafugaji watahakikishiwa masoko pamoja na huduma mbalimbali za mifugo kupitia wataaalamu wa Halmashauri husika.

Katibu Mtendaji wa Mfuko Kichocheo wa SAGCOT Bwa. John. J. Kyaruzi ( kushoto) akisaini makubaliano na Muasisi wa Bothar Bwa. Peter Ireton .
Bwa. John. J. Kyaruzi na Bwa. Peter Ireton wakibadilishana hati za makubaliano.
Mkurugenzi wa huduma za nje ya Nchi wa Bothar,Dkt Bernard Muyeya akitoa maelezo kwa wajumbe namna shirika hilo linavyotoa huduma zake.

Related

kitaifa 6199756034152232308

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item