Msanii wa Nigeria, Ycee kutua Tanzania Jumapili | LUKAZA BLOG

Msanii wa Nigeria, Ycee kutua Tanzania Jumapili

YCEE ambaye pia hufahamika kwa jina la Oludemilade Martin Alejo, anatarajiwa kufika jijini Dar es salaam tarehe 28th Agosti 2016 , ikiwa ...

YCEE ambaye pia hufahamika kwa jina la Oludemilade Martin Alejo, anatarajiwa kufika jijini Dar es salaam tarehe 28th Agosti 2016 , ikiwa ni sehemu ya ziara yake yenye lengo la kutangaza nyimbo zake ambazo ni Omo Alhaji, Jagabana' na nyinginezo. Ziara hiyo itaambatana na mkutano wa waandishi wa habari siku ya Jumatatu tarehe 29th Agosti 2016, ikifuatiwa na ziara ya kutembelea vituo mbalimbali vya habari kuanzia tarehe 29th Agosti 2016 mpaka tarehe 1 Septemba 2016.

Msanii huyo aliyepata umaarufu kupitia wimbo wa ' Jagaban ' na ' Omo Alhaji ' amedhamiria kuungana na mashabiki, wazalishaji wa muziki na wasanii mbalimbali hapa nchini  ili waweze kujenga mahusiano imara zaidi.

Pamoja na hayo amesema kuwa, anayo shahuku kubwa juu ya ziara yake kwani hii ni mara yake ya kwanza hapa nchini."Nina hamu sana ya kukutana na mashabiki wangu wa Tanzania, kwa sababu upendo wanaonipa kupitia mitandao ya kijamii ni wa ajabu na nina furaha sana ya kukutana na watu wapya " , alisema.

Baada ya ziara yake nchini Tanzania , YCEE ataenda nchini South Africa kuendelea na ziara yake yakukuza na kutangaza muziki wake, na anatarajia kuachia orodha ya nyimbo mpya baadaye mwaka huu utakao fahamika kwa jina la ‘The First Wave'.

Msanii huyo wa Omo Alhaji 'YCEE' pia ni miongoni mwa wasanii wanaopenda kusaidia jamii kwa kuwafikia vijana wa kiafrika katika masuala ya maendeleo na michezo.

Hivyo katika ziara yake hapa nchini YCEE atatoa msaada wa fedha kwa kituo cha masuala ya umaskini na ukosefu wa upatikanaji wa elimu kwa watoto wa mitaani Kigamboni. Kigamboni Community Center (KCC) , ni kituo kinacho shughulika na masuala ya kutokomeza umaskini, huku kikijikita katika kutoa elimu ya chekechea na msingi kwa watoto ambao wako mbali na upatikanaji wa elimu. KCC pia hutoa fursa nyingine za kujifunza kwa vijana wa Kigamboni, na pia hutoa elimu ya jamii, madarasa ya kuendeleza vipaji na mafunzo ya ufundi stadi. YCEE ameamua kuunga mkono kituo hiki kwa kwa sababu ya kujitolea kwao kukuza vipaji na kujenga upatikanaji wa elimu kwa jamii.

LINKI ZA KUSIKILIZA NA KUTIZAMA NYIMBO ZAKE

Download link for Jagaban (Audio)


Download link for Jagaban (Video)


Download link for Su Mi (Audio)


Download link for Su MI (Video)


Download link for Omo Alhaji  (Audio)


KUHUSU YCEE

Akifahamika zaidi kwa jina analotumia jukwaani ambalo ni YCEE, Oludemilade Martin Alejo kama ilivyoelezwa na BellaNaija ni msanii maarufu Nigeria. Alianza kazi yake ya muziki mwaka 2012 kama msanii chipukizi kabla ya kusaini mkataba  na Tinny Entertainment.

Hata hivyo baada ya kupata nafasi ya kusoma Biokemia katika chuo kikuu cha Lagos aliacha kujishughulisha na masuala ya muziki kwa muda wa miaka miwili mpaka 2015. Alirudi tena katika ulimwengu wa muziki na wimbo wake wa 'Jagabani' na 'Condo' akishirikiana na Patoranking ambao ulimpandisha chati zaidi na kuteuliwa kushindania tuzo za 'Ushirikiano wa Mwaka ' na ' Video bora ya mwaka' kwenye  'Nigeria Entertainment Awards' huko New York.

YCEE alipata umaarufu kimataifa mara baada ya kuteuliwa kushiriki katika mchakato wa ‘Revelation of the Year’ katika tuzo za muziki za MTV Africa Music Awards 2015 , na kuteuliwa tena katika tuzo za ‘Best Artist in African Pop’ mwaka 2015 kwenye tuzo za 'All Africa Music Awards'. Pia alifanikiwa kuibuka mshindi wa tuzo za ‘Rookie of the year’ kwenye  The Headies mwaka huu.

Kwa sasa YCEE yupo chini ya lebo ya Tinny Entertainment, ambapo  anaendelea kukuza muziki wake kibiashara  kupitia wimbo wake mpya 'Sun mi' ambao ni  remix ya ' Condo ' akishirikiana na Khuli Chana wa Afrika Kusini, KiD X , sambamba na  DJ Consequence aliyeshirikiana nae hivi karibuni  katika wimbo mwingine ' In Benz '

Related

Hot Stories 6283651200971242692

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item