MUARUBAINI WA MADEREVA WAZEMBE BADO NI TATIZO DAR ES SALAAM | LUKAZA BLOG

MUARUBAINI WA MADEREVA WAZEMBE BADO NI TATIZO DAR ES SALAAM

 Ni jioni ya leo Agosti 21, 2016, kuona kituo cha Daladala kuwekwa chini ya Daraja la Treni  lililopo Mtoni Mtongani Jijini Dar es Salaa...

 Ni jioni ya leo Agosti 21, 2016, kuona kituo cha Daladala kuwekwa chini ya Daraja la Treni  lililopo Mtoni Mtongani Jijini Dar es Salaam, kama inavyo onekana Pichani ni gari ya Abiria maarufu Daladala linalofanya safari zake kati ya Mbagala rangi tatu na Buguruni lenye namba za Usajili T 233 CUY, likiwa limeegesha chini ya Daraja la Treni lililopo maeneo ya Mtoni  Mtongani ambapo haikufahamika mara moja Abiria hao walikuwa wametoka wapi wakionekana kwa wingi wakiingia katika gari hilo ambapo nihatari kwa abiria hao na mali kwa ujumla,  nijambo la kusikitisha kwa dereva aliyepitia mafunzo na kufanya kituo hapa na kama inavyo fahamika ni Barabara kubwa na magari huwa yakipita kwa kasi yanapoteremka mteremko huo wa kuelekea Mbagara rangi tatu,  alaumiwe nani ? mazowea nikama sheria nikiwa naimani wahusika watachukua hatua kali na kutowa fundisho kwa wengine na leseni zao kuondolewa barabarani na watangwazwe wazembe wote watakao kuwa wazembe na watakao sababisha ajali.
 Abiria wakipanda eneo hilo hatarishi katika mteremko uliopo chini ya Darala la Treni maeneo ya Mtoni Mtongani Jijini Dar es Salaam bila ya kujili kama sehemu hiyo si salama

 Abiria wakipanda

 Pichani ni Gari lenye namba za Usajili T 951 CDZ, linalofanya safari zake kati ya Temeke na Kongowe nalo likipakia Abiria  eneo hilohilo lililopo chini ya Daraja la Treni, Mtoni Mtongani Jijini Dar es Salaam

(PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)

Related

kitaifa 5732394956253836892

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item