RAIS WA SIMBA EVANCE AVEVA ASHIKILIWA NA POLISI KWA KIBALI CHA TAKUKURU, UCHUNGUZI JUU YAKE WAENDELEA | LUKAZA BLOG

RAIS WA SIMBA EVANCE AVEVA ASHIKILIWA NA POLISI KWA KIBALI CHA TAKUKURU, UCHUNGUZI JUU YAKE WAENDELEA

Rais wa klabu ya Simba, Evance Aveva. Na Zainab Nyamka KAMANDA  wa polisi Mkoa wa kipolisi Kinondoni, ACP Chistopher Fuime amet...

Rais wa klabu ya Simba, Evance Aveva.

Na Zainab Nyamka

KAMANDA  wa polisi Mkoa wa kipolisi Kinondoni, ACP Chistopher Fuime amethibitisha kumshikilia rais wa klabu ya Simba, Evance Aveva, na alipoulizwa ni tuhuma gani zinazomkabili kiongozi huyo wa juu kabisa wa wekundu wa Msimbazi alisema ni vizuri swali hilo wakiulizwa TAKUKURU. Tumemshikilia toka juzi jioni na juhudi za kupatiwa dhamana zimeshindikana mpaka dakika hii kwani sisi kazi yetu ni kumshikilia tu ila mamlaka zaidi yapo TAKUKURU.

Aveva anashikiliwa na polisi kwa kibali cha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU lakini bado haijafahamika moja kwa moja anakabiliwa na tuhuma gani huku baadhi ya watu wakidai ni matumizi mabaya ya fedha walizolipwa kutoka Etoile Du Sahel juu ya malipo ya Emanul Okwi pamoja na za Mbwana Samatta ambazo anadaiwa kuzihamisha kutoka kwenye akaunti ya klabu ya Simba.

“Kwa upande wangu siwezi kujua ila kwa maelezo zaidi  TAKUKURU wanaweza wakajua na ni lini huo uchunguzi  utakamilika na kumpeleka mahakamani. Sisi tunamshikilia kwasababu TAKUKURU hawana mahabusu binafsi,  na maswali yote  wangejibu sababu hasa ya kushikiliwa kwa Evance Aveva,” amesema Fuime 

Kwa upande wa TAKUKURU kupitia afisa habari Musa Misalaba amesema kuwa Aveva yupo kwenye mikono salama na wanamshikilia kwa uchunguzi, kwa sasa wanaendelea na uchunguzi kwani sheria inaturuhusu kufanya uchunguzi  na pia tunaruhusiwa kukamata, kupekuwa kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu.


Sauti: Mahojiano kati ya Maulid Kitenge wa EFM Radio na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni pamoja na Msemaji wa TAKUKURU.

Related

Michezo 3853959659827955580

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item