SHINDANO LA KUMSAKA MKALI WA SINGELI LAZINDULIWA DAR ES SALAAAM | LUKAZA BLOG

SHINDANO LA KUMSAKA MKALI WA SINGELI LAZINDULIWA DAR ES SALAAAM

Katikati ni Mratibu wa mashindano hayo  Masudi Kandoro kutoka kampuni ya High Time Marketing and Promotion ambao ndio waandaaji wakuu ...


Katikati ni Mratibu wa mashindano hayo Masudi Kandoro kutoka kampuni ya High Time Marketing and Promotion ambao ndio waandaaji wakuu wa shindano hayo amkzumgumza na wanahabari mapema leo wakati wa kutangaza Shindano hilo(PICHA NA EXAUD MTEI)
 Kwa mara ya kwanza nchini Tanzania na katika Historia ya music hatimaye mashiundano ya kwanza ya kumtafuta mwanamuziki na mwimbaji wa music wa singeli yamezinduliwa nchini mashindano hayo yakilenga kumpata msanii mwenye uwezo wa kuimba music wa kisingeli mashindano ambayo yamepewa jina la STAR WA SINGELI.

Mashindano hayo ya kuimba singeli nchini Tanzania yanalenga kuibua vijana wenye vipaji vya hali ya juu ambao wako mitaani nia ikiwa ni kuwainua na kuwafanya kuwa wanamusic watakaotambulika ndani na nje ya Tanzania huku pia ikiwa ni njia moja wapo ya kutengeneza ajira zenye staha kwa vijana wa Dar es salaam.

Akizungumza na wanahabari wakati akitangaza kuanza kwa mashindano hayo mbele ya wanahabari Masudi Kandoro kutoka kampuni ya High Time Marketing and Promotion ambao ndio waandaaji wakuu wa shindano hilo amesema kuwa mashindano hayo yatafanyika katika Jiji  la Dar es salaam tu na mashindano hayo yamegawanywa katika sehemu nne ambazo ni Kinondoni,Ilala,Temeke,na Kingamboni ambapo kila sehemu kutafanyika mchujo kwa awamu mbili. Ameongeza kuwa awamu ya kwanza itakuwa katika viwanja vya wazi kila sehemu itatoa washindani 12 kisha awamu ya pili sehemu mbili zitaungana katika mashindano ya ndani nya ukumbi
ambapo kinondoni itaungana na ilala wakati temeke ikiungana na kigamboni.
Akizungumza kuhusu fainali na washindi wa shindano ilo la STAR WA SINGELI amesema kuwa fainali za mashindano hayo zitafanyika siku ya jumamosi ya tarehe 10/09/2016 katika viwanja vya Dar Live Dar es salaam kuanzia saa moja usiku ambapo siku ya fainali atapatikana mshindi mmoja kwenye washindi 12 watakaokuwa wanawania nafasi hiyo ambapo mshindi atajinyakulia zawadi ya million kumi.
Wanahabari wakichulkua Taarifa Hiyo
Akizungumzia mgawanyo wa Million Kumi hizo za mshindi wa kwanza amesema kuwa mshindi hatapewa Kiasi icho chote bali kitagawanywa katika maeneo kadhaa ikiwemo kupata usimamizi wa misic chini ya HIGH TIME,Kurekodi album ya music Audio,Kufanyiwa Video tatu zenye viwango vya kimataifa,Kutangaza Music wa mshindi ndani na  nje ya mipakaya nchi pamoja na kupewa kiasi cha Pesa Taslim.

Katika fainali hizo zitakazofanyika Dar Live zinatarajiwa kupambwa na star wa music huo mzee wa Hainaga Ushemeji Man Fongo na wasanii wengine wakali ambao wanaendelea na mazunguzo kushiriki.

Related

Burudani 4177991055853589622

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item