TAMASHA LA WAANDISHI WA HABARI KANDA YA KASKAZINI KUFANYIKA SEPTEMBER 11 | LUKAZA BLOG

TAMASHA LA WAANDISHI WA HABARI KANDA YA KASKAZINI KUFANYIKA SEPTEMBER 11

   Katibu wa TASWA mkoa wa Arusha, Mussa Juma  akiongea na waandishi wa habari Na Woinde Shizza, Arusha Chama cha waandishi wa h...

Image result for TAMASHA LA TASWA ARUSHA  
Katibu wa TASWA mkoa wa Arusha, Mussa Juma  akiongea na waandishi wa habari

Na Woinde Shizza, ArushaChama cha waandishi wa habari za michezo na Burudanimkoa wa Arusha (TASWA ARUSHA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Arusha Media wameandaa  tamasha la 11 la  waandishi wa habari za michezo na burudani kanda ya Kaskazini ambalo litafanyika Septemba 11 katika uwanja wa Generat Tyre.Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu wa TASWA mkoa wa Arusha, Mussa Juma alisema zaidi ya watu 2500 wanatarajiwa kushiriki Tamasha hilo, ambapo kutakuwa na michezo ya Soka, Kuvuta kamba, Mbio za magunia ,Kukimbiza kuku na muziki kuanzia saa nne asubuhi hadi jioni.Juma alizitaja timu ambazo zitashiriki ni TASWA FC kutoka jijini Dar es Salaam, timu ya Radio  ORS kutoka mkoa wa Manyara, timu ya Sunrise Radio, Timu ya chuo cha uandishi habari Arusha, timu ya MJ Radio na timu ya Triple a Radio.Katika tamasha hilo, pia kutakuwa na timu za vyuo vya uandishi habari vya mkoa wa Arusha, chuo cha habari Maalum, Tasisi ya habari na mawasiliano iliyopo maji ya chai, TASWA Arusha.“tamasha litatanguliwa na semina ya siku moja ya wanahabari mkoani Arusha juu ya masuala ya michezo, Utalii wa ndani na umuhimu wa Uwekezaji katika taifa”alisemaMratibu wa Tamasha hilo, Andrea  Ngobole alifafanua kuwa pia kuna timu ambazo zimealikwa ambazo ni Kitambi Noma, Timu ya TANAPA,timu ya TBL Arusha, timu ya PEPSI na Coca Cola na  Wenyeji  timu ya Wazee Klabu.Ngobole alisema Septemba 3, TASWA na Arusha Media watatangaza zawadi kwa washindi, wadhamini wote na Mgeni rasmi.

Related

Burudani 5400290908045226483

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item