Vifaa bora na vya kisasa vinapunguza matukio ya ajali viwandani | LUKAZA BLOG

Vifaa bora na vya kisasa vinapunguza matukio ya ajali viwandani

 Meneja Ugawaji  wa huduma za TBL Group,James Nyoike,amesema kuwa   utumiaji wa vifaa bora na vya kisasa unapunguza matukio ya  ajali sehem...

 Meneja Ugawaji  wa huduma za TBL Group,James Nyoike,amesema kuwa   utumiaji wa vifaa bora na vya kisasa unapunguza matukio ya  ajali sehemu za kazi hususani  viwandani na kuongeza ufanisi wa kazi na kuongeza uzalishaji.
Bw.Nyoike aliyasema hayo wakati wa kupokea magari ya kupakia na kupakua  mizigo (Forklifts) za kisasa zilizonunuliwa na kampuni hiyo kutoka kampuni ya kusambaza vifaa vya viwandani ya Effco Solution Limited.

Alisema kampuni  ya TBL Group inao  makakati kuhakikisha inatumia mitambo ya kisasa na vifaa vya kisasa  kwa ajili ya kulinda usalama wa wafanyakazi wake ikiwemo kuongeza tija na ufanisi katika uzalishaji “Tunapoongelea vifaa vya kisasa hatumaanishi mitambo tu bali hata vifaa vyote vinavyotumika katika kazi ikiwemo magari yanaotumika kusambaza bidhaa zetu na yanaotumiwa na wafanyakazi wetu katika shughuli mbalimbali “.Alisema.  
 Dereva akiendesha moja ya Forklift nne za kisasa zilizonuliwa na kampuni
Madereva wa Forklift wakiwa wanajaribu kuziendesha baada ya kukabidhiwa
Meneja Ugavi na Usambazaji  wa  TBL Group  ,James Nyoike ( wa  Nne kutoka kulia)  na madereva wa kuendesha Forklifts wakimsikiliza  mtaalamu kutoka EFFCO Solution    Donald Luvaga (kushoto), jinsi Forklift za  kisasa aina ya Toyota zilizonunuliwa na kampuni ya TBL zinavyofanya kazi.

Related

kitaifa 2997966764133157095

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item