Barua kwa Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kuhusiana na Paypal | LUKAZA BLOG

Barua kwa Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kuhusiana na Paypal

Kwanza kabisa napenda kuchukua nafasi hii kukupongeza kwa kazi nzito unayoendelea kuifanya ya kuhakikisha unaitengeneza Tanzania Mpya lak...

Kwanza kabisa napenda kuchukua nafasi hii kukupongeza kwa kazi nzito unayoendelea kuifanya ya kuhakikisha unaitengeneza Tanzania Mpya lakini pia nikupongeze sana kwa namna ambavyo umekuwa ukionyesha nia ya kutaka kuitengeneza nchi hii ambayo kiukweli kuna baadhi ya watanzania walikata tamaa ya kuishi.

Mh Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh John Pombe Joseph Magufuli, Napenda kukufikisha ujumbe huu ambao najua kabisa kuwa wewe ni mmoja kati ya wasomaji wangu wazuri sana na wapenzi wakubwa wa blog hii na kama hukupitia blog hii leo basi naamini kuwa kuna watendaji wako wazuri watakufikishia ujumbe huu ambao una nia nzuri ya kuendana na Kasi yako na kauli mbiu yako ya HAPA KAZI TU.

Mh Rais, Moja ya vitu unavyopambana navyo ni kuhakikisha vijana wanafanya kazi kwaajili ya kujiiingizia kipato lakini pia Taifa liweze kunufaika kupitia kazi wanazofanya. Moja ya Sehemu ya njia ya Serikali kunufaika ni kupitia kodi inayolipwa kupitia huduma na bishaa mbalimbali.

Leo Nimekuja na Hii Kitu inaitwa PAYPAL, Mh Rais naamini kabisa kuwa unafahamu kitu hiki kinachoitwa PAYPAL au ushawahi kuisikia huduma ya PAYPAL.

PAYPAL ni huduma ya malipo ya kidigitali (Electornic pay service) inayotolewa na Kampuni ya Kimarekani ambapo awali ilikua na ubia na kampuni ya Ebay ambapo sasa wamejitenga na kuwa kampuni inayojitegemea. Mh Rais huduma ya PAYPAL ni moja kati ya huduma nzuri sana hapa duniani kutokana na namna tu ya malipo yanavyofanyika kwani Kwa uzoefu wangu ni njia salama na yenye kuaminika sana katika malipo ya kimtandao na yenye kutumika nchi nyingi zaidi barani afrika na hata huko ulaya. Mfano wa nchi ya Afrika ambayo inatumia huduma hii ni Majirani zetu KENYA.

Mh Rais, Huduma ya Paypal ni huduma ambayo mtu anakuwa na uwezo wa kupokea malipo kwa muda mfupi tu pindi anapotumiwa kutoka kwa mtumiaji mwingine wa paypal na pindi mtu anapotumiwa pesa basi huwwa kuna malipo kiasi yanakatwa kwa aliyetumiwa pesa na pindi anapowithdraw au kutoa pesa basi kuna malipo pia yanafanyika kwa hiyo kufanya bank husika kupokea kodi ya pesa inayotolewa na mteja husika hio ni faida kwa nchi kwasababu Kodi itakuja serikalini.

Mh Rais, tuna vijana wengi sana hapa nchini ambao ni wajuzi wa Maswala ya IT, Uchoraji, Wauzaji wa bidhaa kama vinyago, na wengine ni wataalamu wa kuandika makala, Ushauri (Consultant) na vingine vingi tu. Mfano mzuri ni Mimi mwenyewe niliyekuandikia barua hii ni mmoja kati ya wajasiliamali wa mtandao ambapo kuna kazi nyingi sana tunaweza kuzifanya kupitia mitandao na kupata malipo na asilimia kubwa ya malipo hufanywa kwa njia ya PAYPAL ambayo Tanzania hatuna.

Mh Rais, Huduma hii ikiruhusiwa kutumika nchini kama nchi nyingine zinavyotumia huduma hii basi na hizi ndio faida zake 

1: Kutakuwa na watumiaji wengi wa banks ambapo huduma hii ikiruhusiwa kufanyika na Benki kuu ya Tanzania bank zitaweza kuingia ushirikiano na PAYPAL ambapo ukitumiwa pesa kuitoa ni lazima uende bank kwa hiyo watumiaji wa maswala ya kibenki wataongezeka na kuongeza mapato kwa serikali kutokana na kodi ya VAT kukusanywa kupitia utoaji wa pesa hizo kwenye bank husika.

2:Vijana wengi sana na mimi nikiwemo tutaweza kufanya kazi kimataifa kwa kukaa kwenye komputya zetu na hatimaye kuingiza kipato ambacho kitaongeza pato la mtu mmoja mmoja lakini pia Maisha kuboresheka kutokana na kiwango cha pesa tutakachoingiza

3:Watu wengi wataweza kupata kazi ya kufanya kutokana na fursa nyingi sana kupitia mitandao ambayo inaruhusu freelancer kufanya kazi na kulipwa huku watu wakiweza kujiingizia kipato cha ziada na kuboresha maisha yao.

4:Kutachangia kwa asilimia kubwa Matumizi sahihi ya mtandao ambapo watu wengi wataweza kutafuta kazi za kufanya kupitia mitandao na kujiingizia kipato ambacho kitaweza kuboresha maisha ya mmoja mmoja na hatimaye mabank kukusanya kodi pindi pesa zitolewazo na wateja husika.

5: Kutachangia maendeleo ya taifa na watu binafsi pia kutokana na kuwa na wigo mpana wa kuuza bidhaa zetu kupitia mtandao na kufanya kuongeza masoko ya bidhaa zetu kama Vinyago nk.

Mh Rais, Nakuomba kwa nia yako njema uliyo nayo juu ya wananchi wako na mimi nikiwemo, nakuomba sana sana kuweza kuwapa taarifa hii watu husika ambao kwanza Ni Benki Kuu Ya Tanzania kuweza kulifanyia kazi Jambo hili kwa uharaka ili kuweza kuanza kufanya kazi na hatimaye watanzania kuweza kufurahia huduma hii ambayo itaongeza tija kwa taifa na wananchi wake. lakini pia Nakuomba Mh Rais, Kuwapa kazi Benki Kuu ya Tanzania kwanza kufuatilia kwa ukaribu swala hili kama unavyojua kuwa teknolojia inakimbia kwa spidi ya umeme na tusingependa kubakia nyuma sana Ushauri wangu ni kwamba Benki Kuu wanauwezo wa kukutana na wadau na kuweza kujadili hili na namna ambavyo linaweza kuwa na tija kwa Taifa.

Mh Rais najua una majukumu mengi sana ya kutimiza ili kuijenga Tanzania mpya lakini naomba nisikuchoshe kwa barua ndefu huku lengo likiwa tayari limeshafika nipo tayari hata kutoa mawazo yangu pindi yatakapohitajika na wahusika pindi watakapokuwa tayari kulifanyia kazi swala hili. Na naamini wapo vijana wengi ambao tunaweza kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania katika kushauriana na kutoa mawazo chanya katika kufanikisha hili.

Naomba Mh Rais kama hutopata nafasi ya kuisoma hii barua basi nawaomba watendaji wako waliopata nafasi ya kuisoma hii waweze kukufikisha japo upate kufahamu nini wananchi wako tunatamani huduma hii nzuri.

Nikutakie Kazi Njema na yenye mafanikio huku masikio yetu yakiwa tayari kusikia mtazamo wa Benki Kuu ya Tanzania kuhusiana na huduma hii ya PAYPAL.

Related

Makala 7282466244358499590

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item