Hilary Clinton augua ugonjwa wa homa ya mapafu katika kumbukumbu ya wahanga | LUKAZA BLOG

Hilary Clinton augua ugonjwa wa homa ya mapafu katika kumbukumbu ya wahanga

Image caption Bi Clinton akisaidiwa kuingia katika gari Mgombea Urais kutoka chama cha Democratic Hillary Clinton amegundulika kuwa na ug...

Bi Clinton akisaidiwa kuingia katika gari
Image captionBi Clinton akisaidiwa kuingia katika gari
Mgombea Urais kutoka chama cha Democratic Hillary Clinton amegundulika kuwa na ugonjwa wa homa ya mapafu baada ya kuugua katika tukio la kuwakumbuka wahanga wa shambulio la septemba 11.
Daktari wake Lisa Bardack amesema kuwa bi Clinton amekutwa na ugonjwa huo tokea Ijumaa.
Akijerea baada ya kupata nafuu
Image captionAkijerea baada ya kupata nafuu
Amesema pia Clinton aliongezeka joto na kuishiwa na maji mwilini katika tukio hilo la kuwakumbuka wahanga wa shambulio la septemba 11.
Clinton aliondoka mapema, picha zilizowekwa mtandaoni zinamuonesha akisaidiwa na msaidizi wake, huku akitaka kuanguka alipokaribia kwenye gari, lakini baadae bi clinton alitokea kwenye nyumba ya mwanae na kuwaambia waandishi wa habari kuwa anajisikia vizuri.
Donald Trump alihudhuria hafla hiyo
Image captionDonald Trump alihudhuria hafla hiyo
Awali mgombea Urais kupitia chama cha Republican Donald Trump alionesha wasiwasi juu ya afya ya hasimu wake.
Katika shughuli hiyo majina karibu elfu tatu ya wahanga wa shambulizi la Septemba 11 yalisomwa.

Related

Kimataifa 3466291015618451581

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item