Kamoga Mkurugenzi mteule wa Wilaya ya Mbulu aamua kuanza na Mungu | LUKAZA BLOG

Kamoga Mkurugenzi mteule wa Wilaya ya Mbulu aamua kuanza na Mungu

Mkurugenzi mteule wa Wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga, ambaye ameteuliwa mwishoni  mwa wiki jana amesema anaamini ni Mungu aliyemuweka kwen...

Mkurugenzi mteule wa Wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga, ambaye ameteuliwa mwishoni mwa wiki jana amesema anaamini ni Mungu aliyemuweka kwenye nafasi hiyo ili  awatumikie wananchi wa Mbulu kwa wakati huu. 

Akiongea kwenye ibada ya Jumapili hii  ndani ya  Kanisa la Living Water Center Kawe, wakati alipopewa nafasi na mtumishi wa  Mungu  Apostle Onesmo Ndegi  ili asalimia  Kanisa Mheshimiwa Kamonga  alisema, anakwenda kwenye wilaya yenye changamoto nyingi za kimaendeleo ila anaamini Mungu atamwezesha kuzitatua kwa nafasi yake akishirikina na wananchi pamoja na  viongozi wengine kati halimashauri ya Mbulu.


Kamonga alisisitiza kuwa kwa kupata  nafasi hii ya  Ukurugenzi bado  ataendelea na utumishi wake kwa Mungu maana anaamini huo ndio uliomfanya kufikia hatua hiyo,hivyo kuamua kuwa anamtanguliza Mungu kaika kila atakachokuwa anafanya,alisema Kamoga

Pia alitoa shukurani za dhati kwa Mtumishi wa Mungu Apostle Ndegi pamoja
na  watumishi wengine kanisani hapo na kusema kuwa kati ya vitu ambavyo
hawezi kuvisahau na malezi mazuri ya kiroho pamoja na mafindisho ambayo
amekuwa akiyapata kutoka  kwa Apostle Ndegi na watumishi wengine
kanisani hapo, akisema mafundisho hayo yamesababisha kuwa vile alivyo sasa! Mwisho Mtumishi wa Mungu Mtume Onesmo Ndegi  na waumini walifanya maombi kwa ajili yake ili Mungu aambatane naye katika utumishi wake kwenye nafasi hiyo ya Ukurugenzi!.
Mkurugenzi mteule wa Wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga
Mkurugenzi mteule wa Wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga akiwa na Baba yake wa Kiroho Apostle Onesmo Ndegi Kiongozi wa Kanisa la Living Water Center Kawe akimsiliza kwa makini akielezea uteuzi wake.
Mkurugenzi mteule wa Wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga akiwa na Baba yake wa Kiroho Apostle Onesmo Ndegi Kiongozi wa Kanisa la Living Water Center Kawe akimsiliza kwa makini akielezea uteuzi wake.
Apostle Onesmo Ndegi Kiongozi wa Kanisa la Living Water Center Kawe akimwombea Hudson Kamogaakiwa amepiga magoti
Waumini wa Kanisani Living Water Center Kawe wakiwa wamenyoosha mikono kwa Hudson Kamoga kuomba kwa ajili yake

Related

Hot Stories 6718663453525116731

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item