Leo yetu:Utawezaje kutambua Mbwa halisi aina ya Germany Shepherd (Pure Germany Shepherd Dog) | LUKAZA BLOG

Leo yetu:Utawezaje kutambua Mbwa halisi aina ya Germany Shepherd (Pure Germany Shepherd Dog)

Huyu ni mbwa aina ya wolfdog ambapo watu wengi wasio na ufahamu wa mbwa wanaweza kusema kuwa ni pure germany shepherd, na sababu ya wao k...

Huyu ni mbwa aina ya wolfdog ambapo watu wengi wasio na ufahamu wa mbwa wanaweza kusema kuwa ni pure germany shepherd, na sababu ya wao kusema hivyo ni kwasababu tu ya muonekano wake unafanana sana na germany shepherd, masikio, rangi pia ambayo ndio imezoeleka sana ambapo rangi hizo ndio upelekea watu kusema kuwa aina hii ni germany shepherd.

Utakubalia na mimi kuwa Kwa watanzania wengi wasiokuwa na ufahamu na maswala ya Mbwa kila wanapoona Mbwa wa aina flani amabe anafanana na Germany Shepherd basi wao husema ni Germany Shepherd wanashindwa kutofautisha kati ya Pure Germany Shepherd breed na Cross breed ya Germany Shepherd.

Pure GSD ni mbwa ambae amezaliwa akiwa na Asilimia 100 ya vina vya germany shepherd yaani baba ni pure germany shepherd na mama ni pure germany shepherd hivyo mtoto anayezaliwa ni lazima atakuwa pure GSD.

Sasa basi inapotokea Baba ni Pure GSD na Mama ni Pure Rotweiller mtoto hatokuwa pure GSD wala hatokuwa pure Rotweiller bali atakuwa cross breed ya GSD na rotweiller japokuwa mtoto huyo anaweza kuwa na asilimia kubwa ya GSD au Rotweiller inategemea na uwezo wa mbegu umetoka wapi kati ya baba au mama.

Leo tutaweka hapa njia kadhaa za kuweza kufahamu kuwa huyu mbwa ni pure germany shepherd na sio cross breed ya germany shepherd, Kutokana na kutokujua huku watu wengi wametapeliwa kwa kuuziwa mbwa ambao sio pure germany shepherd na kuambiwa ni pure. ZIfuatazo ndio njia ya kutambua kuwa Huyo mbwa ni GSD pure.

1:Kuwa na Muinamo (Bending).
Mbwa aina ya germany shepherd halisi (pure gsd)Hii ni moja ya njia kubwa sana ya kutambua kuwa mbwa huyu ni pure gsd kwanza anakuwa anatengeneza aina flani ya mlima ambayo inaanzia mkiani kupandisha kwenye kichwa ambapo kunakuwa kama kuna kamlima kama anavyoonekana pichani.

Kubend huku ndio sifa moja pekee ya mbwa halisi aina ya Germany Shepherd.
2:Mkia kuburuza chini 
Mbwa halisi aina ya Germany shepherd utamtambua mkia wake unakuwa kama ubaruzika chini kama ambavyo unaona kwenye picha hapo juu na hii ni kutokana na kuwa na umbile kama la mlima linalomfanya aweze kuburuza mkia chini wakati anapotembea mbwa ambae ni cross breed ya germany shepherd hana hio sifa.Kama anayao unaweza share nasi hapa.

3:Masikio kusimama na kuwa kama Pembetatu.
Hii ni moja ya sifa ya mbwa aina ya germany shepherd halisi japokuwa sifa hii wanazo pia aina nyingine mbwa ikiwemo cross breed ya germany shepherd. Kwa sifa hii haitoshi kabisa kusema mbwa huyu ni pure gsd bila kuwa na sifa nyingine.Angalia picha chini jinsi masikio yao yanavyokuwa
4:Rangi Miguuni.
Mbwa halisi aina ya germany shepherd hana rangi mbili miguuni yaani soski(kuna na rangi inayoanzia chini ya miguu hadi katikati ya miguu) mbwa halisi anakuwa na rangi moja tu kuanzia miguuni hadi kwenye mapaja au tumbo na kama ana rangi nyingine basi inakuwa sio kama soski.tazama picha chini unaweza kuona rangi zilizoanzia kwenye miguu kwenda juu ni rangi moja tu kama ni brown ni brown kama ni nyeusi ni  nyeusi tu.
Huyu ni Pure germany shepherd mwenye rangi nyeusi mwanzo mwisho.
Unaweza kuona rangi kwenye miguu yake ni moja tu kuanzia chini mpaka kwenda juu na hii ndio sifa nyingine ya pure gsd

5:Mdomo Kuchongoka
Mbwa hawa wana mdogo uliochongoka japo sio sana lakini unaweza kuona mdomo wake unavyofanana
Unaweza kuona mdomo wa mbwa huyu aina ya german shepherd japokuwa aina nyingine wanaweza kuwa na mdomo wa aina hii hata cross breed lakini pia asiwe pure gsd.

 ili mbwa huyu aweze kuitwa pure germany shepherd ni lazima awe na sifa hizi tulizozitaja hapo juu ila kubwa sana na zaidi ni hiyo ya kubend endapo utaona mbwa wana rangi kama hizo wapo hivyo na sifa nyingine isipokuwa bending basi huyo sio pure germany shepherd bali anaweza kuwa ni cross breeding.

Kwa leo tuishie hapa ....Kama una sifa nyingine unaweza kushare na sisi kwenye comments hapo chini na sisi tutaziweka na kuzifanyia kazi yote ni katika kuhakikisha tunahabarishana na kufundishana kuhusiana na maswala haya ya mbwa

Tufollow facebook, Josephat Lukaza instagram @lukazablog na Youtube MultiLukaza channel.

Related

Makala 1610927904825897274

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item