MAKAMU WA RAIS AWASILI MKOANI MTWARA TAYARI KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU 4 | LUKAZA BLOG

MAKAMU WA RAIS AWASILI MKOANI MTWARA TAYARI KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU 4

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akisalimiana na wananchi waliojitokeza kumsalimia aliposima...


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akisalimiana na wananchi waliojitokeza kumsalimia aliposimama  Nangurukuru, wilaya ya Kilwa mkoani Lindi wakati akiwa njiani kuelekea  mkoa wa Mtwara ambapo atakuwa na ziara ya kikazi ya siku nne.

Sehemu ya Wakazi wa Nangurukuru mkoani Lindi wakishangilia ujio wa Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akisalimiana na wananchi waliojitokeza kumsalimia alipowasili  kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ambapo atakuwa na ziara ya kikazi ya siku nne.
                                     .......................................................... 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema serikali itatuma kikosi maalum cha kukabiliana na uvuvi haramu unaoendelea katika bahari  ili kudhibiti na tatizo hilo ambalo limeathiri sana mazalia ya samaki na kuchangia kupungua kwa samaki baharini.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo 7-Sept-2016 wakati akisalimiana na wananchi wa Nangurukuru wilayani Kilwa mkoani Lindi ambao walijitokeza kumsalimia wakati akielekea mkoani Mtwara katika ziara yake ya kikazi ya siku NNE mkoani huo.Makamu wa Rais amesema katika kuhakikisha kazi hiyo inafanyika vizuri serikali pia itatuma wataalamu wa mazingira ambao watafanya tathmini ya uharibifu wa mazingira katika bahari ili kujua uharibifu uliofanyika na kuchukua hatua ya kukabiliana na hali hiyo.

Ameeleza 
kuwa serikali itachukua hatua hizo ili kuinusuru bahari kwa sababu imekuwa ni 
chanzo kizuri ya mapato kwa wananchi kutokana na shughuli za uvuvi na shughuli 
nyingine zikiwemo za utalii.


“Bahari yetu ndio 
mapato yetu, bahari yetu ndio maisha yetu  
tumeitumia vibaya mapato yamepungua na maisha hayawi mazuri hivyo ni 
muhimu tuitunze ili iendelee kutulea kwa manufaa mazuri.”
Kuhusu 
uboreshaji wa huduma za afya kwa wananchi wa Kilwa, Makamu wa Rais Samia Suluhu 
Hassan amesema serikali inaendelea kuchukua hatua madhubuti zinazolenga 
kuhakikisha wananchi wote nchini wanapata huduma bora za afya katika ngazi 
zote.
Amesema 
mpango huo wa uboreshaji wa huduma za afya kwa wananchi nchini utaenda pamoja 
na utoaji wa elimu bora wa wanafunzi kote nchini chini ya mkakati wa serikali 
wa kutoa elimu bure kuanzia wanafunzi darasa 
la kwanza hadi kidato cha nne.
Katika ziara 
yake mkoani Mtwara, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia 
Suluhu Hassan kesho 8-Sep-16 atazindua
jengo la ofisi  za Tume ya Maadili ya 
Uongozi wa Umma Kanda ya Kusini na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo 
mkoani humo.


Makamu wa 
Rais tayari amewasili mkoani Mtwara na kupokelewa na Viongozi mbalimbali wa 
mkoa huo wakiongozwa na Mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego pamoja na Waziri 
wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angela 
Kairuki.

Related

kitaifa 2429798519104088719

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item