MH. SUBIRA MNGALU AKABIDHI MSAADA WA VIFAA VYA UJENZI KWA AJILI YA UJENZI WA VYOO CHUO CHA MAENDELEO KISARAWE. | LUKAZA BLOG

MH. SUBIRA MNGALU AKABIDHI MSAADA WA VIFAA VYA UJENZI KWA AJILI YA UJENZI WA VYOO CHUO CHA MAENDELEO KISARAWE.

Mbunge wa Viti Maalum CCM kupitia mkoa wa Pwani Mh. Subira Mngalu akikabidhi mifuko ya saruji na vifaa mbalimbali kwa ajili ya ujenzi wa...

01
Mbunge wa Viti Maalum CCM kupitia mkoa wa Pwani Mh. Subira Mngalu akikabidhi mifuko ya saruji na vifaa mbalimbali kwa ajili ya ujenzi wa vyoo kwa Bw.Herry Mjengelaungu Mkuu wa Chuo Cha Maendeleo ya Jamii Kisarawe katika hafla iliyofanyika chuoni hapo leo kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Kisarawe Bw. Mtera Mwampamba na Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Bi. Happiness Saneda.
1
Mbunge wa Viti Maalum CCM kupitia mkoa wa Pwani Mh. Subira Mngalu akizungumza na wakufunzi na wanafunzi wa Chuo Cha Maendeleo ya Jamii Kisarawe kabla ya kukabidhi vifaa katika chuo hicho kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mh. Happiness Saneda.
02
Mbunge wa Viti Maalum CCM kupitia mkoa wa Pwani Mh. Subira Mngalu akipiga picha na mkuu wa chuo hicho pamoja na wakufunzi mara baada ya makabidhiano.
2
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Pwani kupitia CCM Mh. Subira Mngalu akizungumza na Mkuu wa wilaya hiyo Bi. Happiness Sanneda wakati wakikagua maeneo ya chuo hicho kushoto ni Mkuu wa chuo hicho Bw. Herry Mjengelaungu.
3
Mbunge wa Viti Maalum CCM kupitia mkoa wa Pwani Mh. Subira Mngalu akikagua chumba cha kompyuta.
4
Mbunge wa Viti Maalum CCM kupitia mkoa wa Pwani Mh. Subira Mngalu akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Chuo angalia.
5
Mbunge wa Viti Maalum CCM kupitia mkoa wa Pwani Mh. Subira Mngalu akikagua mabweni ya chuo hicho kutoka kwa mkuu wa chuo Bw. Herry Mjengelaungu.
...................................................................................
NA MWANDISHI WETU
MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Pwani, Subira Mgalu(CCM) ametoa msaada
wa vifaa za ujenzi wa vyenye thamani ya sh. milioni moja kwa Chuo
Maendeleo ya Wananchi(FDC) Kata ya Kazimzumbwi, Kisarawe mkoani
Pwani.
Subira alimkabidhi msaada wa vifaa hivyo ambavyo ni
saruji,mchanga,mbao, matofali, nondo na kokoto kwa ajili ya kusaidia
ujenzi wa choo cha wavulana baada ya cha awali kubomoka na wanafunzi
kulazimika kutumia choo kimoja cha wasichana.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo jana, Subira alisema
anaamini ujenzi wa choo hicho utakamilika mapema kwa kuwa unafanywa na
nguvu kazi ya vijana wenyewe chini ya usimamizi wa wakufunzi wao.

Mbunge huyo alisema kwamba anatambua kwamba ana wajibu wa kuhakikisha
afya za vijana wanaosoma chuoni hapo zinakuwa salama hivyo ametoa kama
kiongozi na mzazi wa watoto hao.

Alisema aliguswa baada ya kutembelea chuo hicho mwezi mmoja uliopita
na kuona changamoto nyingi zinazowakabili wanafunzi na watumishi wa
chuo hicho ambapo alihidi kusaidia na kuhamasisha viongozi wengine
wafike chuoni hapo.

Subira alisema vyuo hivyo na vyuo vya ufundi vilivyopo chini ya VETA
ni muhimu hususan wakati huu ambao nchi inaelekea kwenye uchumi wa
viwanda,vyuo hivyo ndivyo vitakavyozalisha wataalamu watakaofanya kazi
kwenye viwanda.

Alisema vyuo hivyo ambavyo kwa Mkoa wa Pwani vipo Kibaha, Kisarawe na
Ikwiriri wilayani Rufiji, miundombinu yake ni chakavu na wanakabiliwa
na changamoto nyingi hivyo wakati serikali inaangalia namna, viongozi
na wadau wanapaswa kusaidia.

Mbunge huyo alimuomba Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happines Senada na
uongozi wa halmashauri kuwatumia vijana wa chuo hicho kuwapa kazi
hususan za ujenzi wa vyoo vya shule za msingi ili kusadia vyuo hivyo
na kwamba sheria ya manunuzi imeruhusu kutumia makundi maalumu ya
vijana na wanawake.

Awali akizungumza na wafanyakazi na wanafunzi wa chuo hicho Mkuu wa
Wilaya, Happines alisema chuo hicho kina umuhimu mkubwa hivyo
atahakikisha changamoto zinazowakabili zinatatuliwa kwa kushirikiana
na wadau.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho Heri Mjengelaungu, alisema chuo
hicho kinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo miundombinu chakavu,
tatizo la maji, umeme, vifaa vua kufundishia kwa vitendo , haina
magari.

Alimshukuru mbunge huyo kwa msaada wake wa vifaa vya ujenzi wa choo
hicho kwa kuwa hali ni mbaya hivyo watahakikisha kwa kushirikiana na
wanafunzi na wakufunzi choo hicho kinakamilika mapema zaidi kwa kuwa
shimo limeshachimbwa.

Related

Kijamii 7450274118961875525

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item