MKUU WA MKOA WA ARUSHA AMPA WIKI MBILI MKURUGENZI WA JIJI KUHAKIKISHA WALIMU WOTE WANAODAI SERIKALI WALIOPO NDANI YA JIJI LA ARUSHA WANALIPWA FEDHA ZAO | LUKAZA BLOG

MKUU WA MKOA WA ARUSHA AMPA WIKI MBILI MKURUGENZI WA JIJI KUHAKIKISHA WALIMU WOTE WANAODAI SERIKALI WALIOPO NDANI YA JIJI LA ARUSHA WANALIPWA FEDHA ZAO

  MKUU wa mkoa Arusha Mrisho Gambo akiongea na  walimu wote wabshule za msingi 48 zilizopo ndani ya Halmashauri ya jiji la Arusha  ,warat...

 MKUU wa mkoa Arusha Mrisho Gambo akiongea na walimu wote wabshule za msingi 48 zilizopo ndani ya Halmashauri ya jiji la Arusha  ,waratibu elimu,wakaguzi elimu pamoja na maafisa elimu kata
 Mkuu wa wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro akiwa anaongea na walimu waliouthuria mkutano huo.Habari picha na Woinde Shizza,Arusha

MKUU wa mkoa Arusha Mrisho Gambo amemuagiza mkurugenzi wa jiji la Arusha Athumani Kihamia kulipa madeni yote wanayodai  walimu ya milioni 154  ndani ya wiki mbili  ambayo wamekuwa wakidai  serikali kuu kwa  muda mrefu bila kulipwa na hivyo kusababisha walimu hao kukata tamaa ya ufundishaji wanafunzi .

Gambo alitioa agizo hilo jana alipokuwa akizungumza na walimu wote wa shule za msingi 48 zilizopo ndani ya Halmashauri ya jiji la Arusha  ,waratibu elimu,wakaguzi elimu pamoja na maafisa elimu kata katika mkutano wa kujua changamoto zinazowakabili walimu hao ili zipatiwe ufumbuzi.

Alisema kuwa walimu wamekuwa wakifundisha katika mazingira magumu na kwamba  hadi sasa wapo walimu wa shule za msingi wanaoadai madeni ya likizo na mengineyo yenye gharama ya milioni 154 ambapo serikali kuu ndio inayopaswa  izilipe na hadi sasa hawajalipwa jambo ambalo linawafanya walimu hao kupoteza muda wa kufundisha na kufuatilia kila siku madeni hayo.

  “mkurugenzi nakupa muda wa wiki mbili deni hili la milioni 154 kwa ajili ya walimu akikisha zinalipwa haraka iwezekanavyo wakishalipwa ndio upambane na serikali kuu ufidie hapo zilikotolewa kwani haiwezekani walimu wapoteze muda kila siku wakifuatilia tu madeni huku wakiwa wameacha vipindi bila kufundisha wanafunzi wetu”alisema Gambo.

Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji hilo,Athumani Kihamia akijibu agizo hilo alilopewa na mkuu wa mkoa alisema kuwa fedha hizo ambazo ni madeni hayo  zinapaswa zitokee serikali kuu na kwamba atahakikisha kuwa ndani ya muda wa wiki mbili atazilipa kupitia fedha za ndani za halamshauri hiyo  ili zikija zirejeshwe.

Alifafanua kuwa deni hilo atalipa kutoka kwenye fedha alizoziokoa ambazo zilikuwa zinalipwa kinyume cha sheria kwa madiwani  ambapo kiasi cha milioni   130  zilizokuwa zinatumika  kuwalipia madiwani mafuta ,simu   pamoja na nauli zitaelekezwa kulipa walimu hao madai yao  ili waweze kujikimu na hali wanayokabiliana nayo.

‘‘Fedha ambazo zimeokolewa kwa ajili ya mafuta ni milioni 40.8,fedha za simu za madiwani milioni 61.2,nauli iliyookolewa milioni 28 ambapo jumla ni milioni 130 ambazo zimelipwa kinyume hivyo fedha hizi zinaelekezwa kwa walimu wa msingi na sekondari ikiwa ni madeni wanayodai halmashuri hii ambapo fedha zinasubiriwa serikali kuu lkni tumeona tuwatangulizie hizi fedha ili wajikimu na waweze kufundisha watoto wetu vizuri”alisema Kihamia .

Kihamia alisema kuwa watatanguliza fedha hizo kwa walimu hao wakati wakiwa wanasubiria fedha toka serikali kuu ili waendelee kujikimu kwani zimeokolewa katika mianya ambayo zilikuwa zinateketea hivyo zitaongeza  ufanisi  kwa walimu  katika kufundisha wanafunzi na akili zao  na kufanya akili zao kuzielekeza kwa wanafunzi ili wapate elimu bora.

Baadhi ya walimu hao wakieleza kero zao walisema kuwa wanakabiliwa na tatizo la kutopandishwa madaraja kwa  waliokaa kazini muda mrefu
huku wengine walioingia kazini muda mfupi  wakiwa wanapandishwa madaraja bila kujua vigezo  hivvyo  kumwomba mkuu wa mkoa kuingilia swala hilo.
 wa kwanza kushoto ni mkurugenzi wa jiji la ArushaAthumani Kihamia akiwa anasikiliza kwa makini malalamiko ya walimu hao
 picha ya juu na chini ni walimu waliouthuria mkutano huo wa mkuu wa mkoa  uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa AICC uliopo mkoani Arusha

Related

kitaifa 649386019885415488

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item