ROBO TATU YA WATU WALIOPO GEREZANI NCHINI TANZANIA SIO WAFUNGWA | LUKAZA BLOG

ROBO TATU YA WATU WALIOPO GEREZANI NCHINI TANZANIA SIO WAFUNGWA

Mkurugenzi  wa Legal Services Facility , ScholasticaJulu, akizungumza na wadau waliofika katika hafla ya miaka mitano ya LSf  Wajumbe...

Mkurugenzi wa Legal Services Facility ,ScholasticaJulu, akizungumza na wadau waliofika katika hafla ya miaka mitano ya LSf
 Wajumbe wa Bodi wa Legal Services Facility katika picha ya pamoja
 Mwenyekiti wa bodi ya Lsf , Joaquine De Mello akiakabidhi hundi kwa mmoja wa wanufaika.
 Mnufaika wa Ruzuku kutoka tasisi ya  TEWORECakinyoosha hundi yake juu yenye thamani ya shilingi bilioni moja
 Wanufaika wa Ruzuku wakiwa katika picha ya Pamoja na Wajumbe wa bodi

Mkurugenzi wa Legal Services Facility ,Scholastica Julu, akizungumza na wadau waliofika katika hafla ya miaka mitano ya LSf


 Mkurugenzi wa Legal Services Facility ,Scholastica Julu, akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa  LSf

Na  Humphrey   Shao, Dar es Salaam

WITO umetolewa kwa wadau wa sheria  kusaidia kupunguza  mahabusu Magerezani kutokana na wingi wao ambao aikuwa lazima kuweka humo .


Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la kisheria lisilo la kiserikali la Legal Services Facility (LSF),Joaquine De Mello,  wakati wa Hafla ya miaka mitano ya shirika hilo na kukabidhi fedha kwa mashirika mapya ya wanaufaika.


“nimeweza kuzunguka magereza yote nchini na kujionea namna gani wafungwa walivyojazana  kwa wingi lakini robo tatu ya wafungwa waliopo humo ni mahabusu ambao awaja hukumiwa” alisema Jaji Joaquine De Mello Aliongeza kuwa  imefika wakati wa wasaidizi wa kisheria kuanza kuwasaidia watu kwa ngazi ya  vituo vya Polisi ambapo huko wanaweza kupata dhamana kabla ya kufika  magerezani.


Kwa upande wake, Scholastica Julu, Mkurugenzi mtendaji wa Shirika hilo alisema kuwa shirika hilo limeweza kutoa fedha zaidi ya Bilioni ishirini kwa mashirika mbalimbali nab ado litaendelea kutoa hili kuweza kusaidia wasaidzi wa kisheria na Mashirika yanayowasimamia .


Alisema kuwa wameweza kupokea changamoto ya usafiri kwenye baadhi ya mikoa na kama shirika wanalifanyia kazi hilo swala hili waweze kutatua tatizo hilo kwa wasaidizi wanaofanya kazi hiyo kwa mazingira hayo magumu. 

Related

kitaifa 8094005924128035692

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item