TBL Group yapiga jeki Wiki ya Nenda kwa Usaalama barabarani | LUKAZA BLOG

TBL Group yapiga jeki Wiki ya Nenda kwa Usaalama barabarani

Katika jitihada za kutokomeza ajali za barabarani nchini,kampuni ya TBL Group leo imetoa vifaa vya uhamasishaji wa usalama  katika wiki ya ...

Katika jitihada za kutokomeza ajali za barabarani nchini,kampuni ya TBL Group leo imetoa vifaa vya uhamasishaji wa usalama  katika wiki ya Nenda kwa Usalama  barabarani vilevile imekuja na huduma mpya ya kupima afya za madereva ya zahanati inayotembea ‘Zahanati Mwendo’.
 
Akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa hivyo,Afisa Mawasiliano wa TBL Group,Amanda Walter,alisema kuwa msaada huu ni mwendelezo wa kampuni kushiriki katika kampeni za  Usalama barabarani.
 
“TBL Group ikiwa ni kampuni inayotengeneza vinywaji vyenye kilevi kwa muda mrefu tumekuwa tukifanya kazi na serikali kupitia Jeshi la polisi katika kampeni za kuhamasisha usalama barabarani lengo kubwa likiwa ni kutokomeza matukio ya ajali nchini kupitia kampeni yetu ya usalama na Unywaji wa Kistaarabu”.Alisema Amanda.
 
Alivitaja vifaa vya uhamasishaji usalama katika Wiki ya Nenda na Usalama Barabarani kuwa ni Stika 1,000,Tisheti 1000 na kofia 500 na imewezesha upimaji wa afya za madereva kupitia Zahanati Mwendo “Huduma hii ni gari maalumu lenye vifaa vya kupima afya za madereva na wataalamu wa afya na litakuwa linazunguka sehemu mbalimbali nchini kwa ajili ya kupima afya za madereva na kuwapatia matibabu na huduma hii itakuwa inapatikana bure kuanzia sasa hadi mwanzoni mwa mwezi ujao na tutaendelea kufanya kampeni zaidi”.Alisema.
 
Kwa upande wake Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani wa Jeshi la Polisi,Kamanda Mohamed Mpinga ,kwa niaba ya  serikali aliishukuru TBL Group na wadau wengine ambao wanashirikiana na jeshi hilo kufanikisha kampeni za usalama barabarani.

Alisema bado kuna matukio mengi ya ajali nchini ambazo zinasababisha vifo vya watu wengi na kuleta hasara nyingi hivyo kunatakiwa jitihada za pamoja kufanya kampeni ya kuzipunguza ikiwezekana hata kuzimaliza kabisa.

“Mwaka huu TBL Group wamekuja na huduma ya kupima afya za madereva kupitia Zahanati inayotembea ambayo ni ya aina yake nchini hivyo natoa wito kwa madereva wote watakapoona gari hili maalumu litakalozunguka sehemu mbalimbali wajitokeze kupima afya zao na kutakuwepo na vipimo vya macho,shinikizo la damu ,sukari na vinginevyo tena vinatolewa bure”.Alisema Kamanda Mpinga.

Wiki ya Usalama barabarani itafikia kilele wiki ijayo ambapo itafanyika kitaifa mkoani Geita.
 Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani wa Jeshi la Polisi,Kamanda Mohamed Mpinga akiongea wakati wa hafla ya kupokea vifaa vya uhamasishaji katika Wiki ya Nenda kwa Usalama barabarani kutoka kampuni ya TBL Group,katikati ni Afisa Mawasiliano wa kampuni hiyo,Amanda Walter na kushoto ni Mkurugenzi wa huduma za Zahanati Mwendo,Rosemary Mwakitwange.
 Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani wa Jeshi la Polisi,Kamanda Mohamed Mpinga akimpongeza Afisa Mawasiliano wa kampuni hiyo,Amanda Walter baada ya kutembelea gari la kupima afya za madereva
 Kamanda mpinga akipokea baadhi ya vifaa vya uhamasishaji usalama vilivyotolewa na TBL Group
Afisa Mawasiliano wa kampuni hiyo,Amanda Walter,akiongea wakati wa hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Related

Kijamii 8818493486421313296

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item