TETEMEKO LA ARDHI LAZUA TAHARUKI KANDA YA ZIWA | LUKAZA BLOG

TETEMEKO LA ARDHI LAZUA TAHARUKI KANDA YA ZIWA

Nyumba kadhaa Mkoani Kagera zimebomoka baada ya tetemeko la Ardhi lenye nguvu ya 5.7 kipimo cha Ritcher kupita kwenye mikoa hiyo ya Kanda...

Nyumba kadhaa Mkoani Kagera zimebomoka baada ya tetemeko la Ardhi lenye nguvu ya 5.7 kipimo cha Ritcher kupita kwenye mikoa hiyo ya Kanda  ya Ziwa. Taarifa zinadai Mji wa Kamachumu Mkoani Kagera ndio umeathiriwa Vibaya na tetemeko hilo, ambapo nyumba nyingi zimebomolewa.

Hadi sasa hakuna idadi ya vifo au Majeruhi iliyotolewa na Mamlaka zinazohusika mkoani Kagera.


Nyumba Moja wapo ambayo imeathirika na Tetemeko hilo lililotokea Muda mfupi uliopita Mjini Bukoba.

Nyumba ikionekana kupata nyufa baada ya tetemeko la Ardhi kuutikisa Mji wa Bukoba hivi Punde

Milango ya Geti katika nyumba hiyo ikionekana kuanguka chini baada ya kukumbwa  na dhoruba ya tetemeko la Ardhi, lililotikisa Mji wa Bukoba.
Baadhi ya Nyumba za Wananchi wa Mji wa Bukoba Zikiwa katika hali Mbaya baada ya Tetemeko la Ardhi Kupita.

Gari ya Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji Mjini Bukoba likiwa katika harakati za Uokoaji. 

Related

Hot Stories 6682183581054130579

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item