Topic yetu ya leo tunamuangaza Germany Sherpherd Dogs...Wapendwao sana. | LUKAZA BLOG

Topic yetu ya leo tunamuangaza Germany Sherpherd Dogs...Wapendwao sana.

Mbwa aina ya Germany Shepherd  Asili ya Mbwa huyu imetokea nchini Ujerumani na aina hii ikatambulika rasmi kuwa ni Germany Sherpherd ...

Mbwa aina ya Germany Shepherd 

Asili ya Mbwa huyu imetokea nchini Ujerumani na aina hii ikatambulika rasmi kuwa ni Germany Sherpherd Dog kwa Kiingereza huku Nchini Britania akijulikana kama  Alsatian. Aina hii ni kama aina mpya ya mbwa ambayo uhalisia wake ulipatikana mnamo mwaka 1899.
Mbwa aina ya Germany Sherpherd akifundishwa kuruka viunzi na Askari wa Jeshi la Marekani.

Uhalisia wa mbwa uliendelezwa ili kuwa na lengo moja kuu tu la kuchunga kondoo. Kutokana na uwezo wake, kuelewa kwake, kuwa na akili kupitiliza, na nidhamu ndio ikapelekea mbwa hawa kutumiwa kwa kazi nyingi kama vile kusaidia walemavu, tafuta na okoa, na kazi zote za kijeshi pamoja na uigizaji. Germany sherpherd ni breed ya pili kubwa maarufu  nchini Marekani na Breed ya nne kubwa maarufu nchini Uingereza.

Vilevile Aina hii ya Mbwa ni breed ya kwanza kubwa sana hapa nchini Kwetu  kwa ujumla, umaarufu huu umetokana na uwezo wa mbwa huyu kufanya kazi mbalimbali, uaminifu na pamoja na umbo na rangi inayopatikana kwa mbwa hawa.
Mbwa hawa wamekuwa maarufu sana nchini Kwetu kutokana na uonekano wake katika kazi wanazotumiwa na Jeshi la Polisi katika kazi zake kama Kutuliza ghasia na kupelekea watu wengi kusema wanapenda kuwa na mbwa wa polisi bila kufahamu kuwa mbwa hawa wanafundishwa kwaajili ya shughuli maalumu.

Mbwa hawa wana uwezo mkubwa sana pale wanapofundishwa kuhusiana na kazi flani ambapo wanaweza kufundishwa kuokoa watu, au kuhakikisha wanatuliza ghasia kama ambavyo polisi wanawatumia. Lengo la Polisi kuwatumia hawa ni kwasababu zifuatazo

Moja ni kwamba Mbwa aina ya Germany Sherpherd wana akili sana na pindi wanapofundishwa uelewa kwa muda mfupi sana na ndio maana Mbwa hawa wanapendwa sana sana na watu wengi hapa nchini.

Pili Mbwa hawa wanapofundishwa wanakuwa na uelewa mkubwa kutoka kwa master wake au trainer na pindi anapoamuliwa kufanya kitu flani ni rahisi kuambiwa acha kufanya na akaacha kabla ya kufanya alichoambiwa tofauti na mbwa kama doberman ambaye akiamliwa kufanya kitu kama kuvamia hata umkataze wakati kashaenda hawezi kurudia njiani. lakini pamoja na sifa zote mbwa aina ya german sherpherd ana tabia moja tu ya uaminifu kitu ambacho kinafanya apendwe uaminifu huo ni kwamba mfano unaweza kumkataza asimng'ate mtu na akafanya hivyo tofauti na mbwa wengine ambao unaweza kumkataza ila baada ya sekunde kadhaa tu akamvamia na kumng'ata na ndio maana polisi  wanapenda kuwatumia hawa kwasababu hata atakapomuru kwenda kumkamata tu mtu basi na atafanya hivyo na pengine asimdhuru huyo mtu aliyetumwa kumkamata.

Mbwa hawa ni moja kati ya aina z mbwa ambao unapowafuga unahitaji kuwa mwangalizi wa hali juu kuhusiana na Matunzo, afya na aina ya vyakula japokuwa mbwa anaweza kula chochote ambacho binadamu anakula kikubwa kikiwa kwenye hali nzuri.

Vilevile Watu hutokea kuwapenda aina hii ya mbwa na ndio maana wengi utawasikia napenda mbwa kama wa polisi kitu ambacho wengi wakimaanisha aina ya mbwa na sio kazi anayofanya. Mbwa anaweza kufundishwa vile unavyotaka wewe na akawa na ndio maana mbwa wanaonusa madawa ya kulevya hawawezi kumkimbiza mtu wala sio wakali. Kwa hiyo mbwa anaweza kuwa vile unavyotaka lakini mara nyingi hutegemea na aina flani ya mbwa ambapo huwa ni rahisi sana kufundishika kuhusu maswala flani kama ulinzi, ukoaji na ndio maana mbwa wengi wanaotumika katika ukoaji, kutafuta na kusaidia walemavu germany sherpherd ndio anatumika kutokana na sifa zake hizo kama uaminifu na mwenye kuwa karibu sana na trainer wake.

Najua mpaka sasa utakuwa ushamwelewa sana aina hii ya mbwa na kama unachochote unaweza kushare nasi katika kuendeleza kujifunza juu ya mbwa hawa.

Tufollow kwenye facebook kwa Jina la Josephat Lukaza, Instagram @lukazablog na twitter Lukaza2010. kuendelea kupata tips mbalimbali kuhusiana na mbwa.

Related

Makala 8979029691497651945

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item