Waandishi wa habari wanawake Mbeya watembelea kiwanda bora cha bia barani Afrika | LUKAZA BLOG

Waandishi wa habari wanawake Mbeya watembelea kiwanda bora cha bia barani Afrika

Meneja wa kiwanda cha TBL Mbeya,Jemedari Waziri akiongea na ujumbe wa waandishi wa habari waliotembelea kiwanda Mtaalamu wa Mafunzo w...

Meneja wa kiwanda cha TBL Mbeya,Jemedari Waziri akiongea na ujumbe wa waandishi wa habari waliotembelea kiwanda
Mtaalamu wa Mafunzo wa Kiwanda cha Bia cha TBL- Mbeya, Christian Kivyiro akitoa maelekezo kwa waandishi wa habari wanawake wa Mkoa wa Mbeya, walipotembelea kiwanda hicho jana ili kujifunza namna kinavyofanya kazi
Mtaalamu wa Mafunzo wa Kiwanda cha Bia cha TBL- Mbeya, Christian Kivyiro akiwaonyesha Shahiri waandishi wa habari wanawake wa Mkoa wa Mbeya, walipotembelea kiwanda hicho ili kujifunza namna kinavyofanya kazi
Waandishi wakiwa pichani wakiwa wameshikilia ngao na cheti cha tuzo za ushindi wa kiwanda bora barani Afrika
Fundi Sanifu wa maabara ya kiwanda cha Bia cha TBL-Mbeya, Phili Said (kulia) akitoa maelekezo namna pombe inavyopimwa katika maabara yao kwa waandishi wa habari wanawake wa Mkoa wa Mbeya.
-Wafurahia mafanikio yake
Siku chache baada ya kiwanda cha bia cha TBL Mbeya kutangazwa kuwa kiwanda bora barani Afrika,pongezi kwa mafanikio hayo zimekuwa zikitolewa kutoka makundi mbalimbali ya kijamii mkoani humo na kupokea maombi ya kutembelewa kwa ajili ya mafunzo na kujionea jinsi kinavyoendesha shughuli zake.
Moja ya kundi lililoguswa na mafanikio hayo na kutembelea kiwanda hicho ni wanachama kutoka Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake mkoani humo ambao baadhi ya wanachama wake wametembelea kiwanda na kupata fursa ya kutembezwa idara  mbalimbali kiwandani hapo na kuongea na Meneja wa kiwanda,Mhandisi Jemedari Waziri.
Waziri aliwaelezea waandishi hao kuwa siri ya mafanikio hayo ni uwekezaji mkubwa uliofanywa na kampuni kuanzia kwenye mitambo ya uzalishaji mpaka kwenye wafanyakazi walioajiriwa na kiwanda bila kusahau mifumo ya uendeshaji viwanda ya kisasa iliyowekwa na kampuni.

Alisema kiwanda kitaendelea kushirikiana na serikali na wadau wengine mkoani humo katika miradi mbalimbali ya kubadilisha jamii hususani katika sekta ya utunzaji Mazingira na kulinda vyanzo vya maji.

Related

kitaifa 8078266744855123169

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item