Wafanyakazi wa TBL wasafisha mazingira Ilala Mchikichini | LUKAZA BLOG

Wafanyakazi wa TBL wasafisha mazingira Ilala Mchikichini

Wafanyakazi wa kampuni ya TBL Group kiwanda cha Ilala jijini Dar es Salaam  jana walitumia sehemu ya muda wao kwa kushiriki kwenye shughuli...

Wafanyakazi wa kampuni ya TBL Group kiwanda cha Ilala jijini Dar es Salaam  jana walitumia sehemu ya muda wao kwa kushiriki kwenye shughuli za jamii ambapo walisafisha maeneo ya Ilala Mchikichini.
 

Zoezi hilo ni moja ya mkakati wa kampuni wa kutunza mazingira kwa vitendo ambapo pia wafanyakazi wake kutoka viwanda vyake vyote nchini mara kwa mara wamekuwa wakishiriki katika shughuli za usafi mara kwa mara.
 Wafanyakazi wa kiwanda cha bia cha Ilala (TBL Group)  wakifanya usafi kwenye mfereji wakupitisha maji machafu uliopo katika Mtaa wa Mission  Kota ya Mchikichini Ilala jijini Dar es Salaam.
 Afisa Mwandamizi wa Kiwanda cha bia cha TBL  Ilala jijini Dar es Salaam, Charles Nkondola (kushoto) akibadilishana mikakati ya usafi na  Diwani wa kata ya Mchikichini Joseph Ngowa ( kulia) . Katikati ni Afisa usalama na Afya wa TBL Group, Khery Gunzarethy.
 Afisa Mwandamizi wa kiwanda cha TBL cha Ilala Charles Nkondola akishirikiana na wafanyakazi wenzake kufanya usafi kwenye mtalo wa kupitisha maji machafu wa Mission uliopo katika kata ya Mchikichini jijini Dar es Salaam
 Wafanyakazi wa kiwanda cha bia cha TBL Ilala jijini Dar es Salaam, wakiongozwa na Afisa usalama na Afya wa TBL Group, Khery Gunzarethy wakifanya usafi kwenye mtalo wa kupitisha maji machafu   uliopo katika kata ya Mchikichini .
Wafanyakazi wa Kiwanda cha bia cha TBL Ilala jijini Dar es Salaam, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kata ya Mchikichini mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kufanya usafi wa mfereji wa Mission Kota .

Related

Kijamii 2266764043167166312

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item