Wananchi kagera kunufaika na mradi wa maji wa TBL Group | LUKAZA BLOG

Wananchi kagera kunufaika na mradi wa maji wa TBL Group

Mkurugenzi Mkazi wa Amref Health Afrika Tanzania Dk.Florence Temu (katikati) na Mtaalamu    wa Maji,Afya na Usafi wa Mazingira wa Amref H...

Mkurugenzi Mkazi wa Amref Health Afrika Tanzania Dk.Florence Temu (katikati) na Mtaalamu  wa Maji,Afya na Usafi wa Mazingira wa Amref Health Afrika- Tanzania Mhandisi Charles Mlingi (kuahoto) wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa TBL GroupGeorgia Mutagahywa, (kushoto)  jijini Dar es Salaam  ,wakati alipokuwa akifafanua jamabo mara baada ya kusaini mkataba wa makubaliano na Amref Health Africa –Tanzania  wa kuchimba kisima cha  maji  katika Wilaya ya Muleba  mkoa wa Kagera.
 Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa TBL GroupGeorgia Mutagahywa, (kulia)   na Mkurugenzi Mkazi wa Amref Health Afrika Tanzania Dk.Florence Temu. wakikabidhiana hati  za makubaliano ya kuchimba kisima cha  maji safi katika Wilaya ya Muleba  mkoa wa Kagera.
Mkurugenzi Mkazi wa Amref Health Afrika Tanzania Dk.Florence Temu (katikati) na Mtaalamu  wa Maji,Afya na Usafi wa Mazingira wa Amref Health Afrika- Tanzania Mhandisi Charles Mlingi (kushoto) wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa TBL GroupGeorgia Mutagahywa, (kushoto)  jijini Dar es Salaam  ,wakati alipokuwa akifafanua jamabo mara baada ya kusaini mkataba wa makubaliano na Amref Health Africa –Tanzania  wa kuchimba kisima cha  maji  katika Wilaya ya Muleba  mkoa wa Kagera.

 Kampuni ya TBL Group imesaini mkataba mkataba na Shirika lisilo la Kiserikali la AMREF Tanzania  kwa ajili ya kuchimba kisima cha maji chenye kina kirefu katika  kijiji cha Busole Wilayani Muleba,mradi wenye thamani  ya zaidi ya milioni 67 ambao ukikamilika utanufaisha wananchi wa kijiji hicho na vijiji jirani.
 
Akiongea wakati wa hafla ya kusaini mkataba huo jijini Dar es Salaam jana,Mkurugenzi wa Mambo  ya Nje wa TBL Group,Georgia Mutagahywa alisema kuwa msaada huo  ni utekelezaji wa moja ya sera ya kampuni ya kutumia sehemu ya faida inayopata baada ya kulipa kodi kusaidia huduma za kijamii.
 
Alisema kampuni  imeingia ubia na AMREF Tanzania katika utekelezaji wa mradi huu kwa kuwa ni moja ya taasisi ambao inao utaalamu wa kutekeleza miradi ya maji vijijini ambayo imeonekana kunufaisha jamii katika sehemu mbalimbali za nchini.
 
Tunafurahi kushirikiana na AMREF katika mradi huu unaotarajiwa kukamilika ndani ya kipindi cha mwaka mmoja,tuna uhakika utawapunguzia wanawake adha ya kutembea mwendo mrefu kutafuta maji,kupunguza utoro wa wasichana mashuleni pia utawezesha wakazi wa maeneo hayo kupata maji safi na kupunguza uwezekano wa kupata maradhi yatokanayo na matumizi ya maji yasio salama”.Alisema Mutagahywa.
 
Alisema  TBL Group ikiwa kampuni inayotegemea malighafi ya maji kwa asilimia kubwa katika viwanda vyake inaelewa changamoto iliyopo ya upungufu wa maji katika sehemu mbalimbali na ndio maana imekuwa ikisaidia kufanikisha miradi ya kuwapunguzia wananchi adha ya maji kwa kusaidia kuwachimbia visima kama ambavyo imefanya katika mradi huu “Tunaelewa tatizo la maji ni  changamoto kubwa na tutaendelea kushirikiana na serikali na wadau wengine kufanikisha miradi ya maji katika sehemu mbalimbali nchini”.Alisema.
 
Kwa  upande wake Mkurugenzi Mkazi wa AMREF Tanzania,Dk.Florence Temu,aliishukuru TBL Group kwa kuamua kushirikiana na taasisi yake kutekeleza mradi wa maji wa kuboresha maisha ya wananchi wa wilaya ya Muleba.

“Tunashukuru kushirikiana na TBL Group katika mradi huu na tutahakikisha tunaufanikisha na unaleta manufaa kwa  wananchi  kama ilivyokusudiwa kwa kuwa tunao  utaalamu na uzoefu wa muda mrefu wa kuendesha miradi ya uchimbaji wa visima vya maji katika maeneo ya vijijini na tumefanikisha uazishwaji wa miradi shirikishi ya maji sehemu mbalimbali vijijini”.Alisema Dk. Temu.
 

Aliongeza kuwa katika  hatua ya awali kampuni itafanya utafiti ili kubaini sehemu ya kuchimba kisima hicho na baada ya kufanikisha zoezi na kuufanya mradi huo kuwa endelevu  itatoa elimu kwa wananchi  ili wauone mradi huu kuwa ni wa kwao hata baada ya kukamilika.

Related

Kijamii 2087851046039335637

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item