Alichokipost Waziri Mwigulu kuhusiana na kupigwa Kwa Mwanafunzi | LUKAZA BLOG

Alichokipost Waziri Mwigulu kuhusiana na kupigwa Kwa Mwanafunzi

Waziri Wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh Mwigulu Nchemba Mnamo Tarehe 28.9.2016, mwanafunzi aitwaye Sebastian Chinguku wa form 3A mbeya d...

Waziri Wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh Mwigulu Nchemba

Mnamo Tarehe 28.9.2016, mwanafunzi aitwaye Sebastian Chinguku wa form 3A mbeya day sec school aishie Uyole alipigwa na walimu watatu, Mwl Frank Msigwa, John Deo UDSM na Sanke Gwamaka wa Nyerere Memorial, wote wakiwa mafunzo. 

Mwl Frank alitoa assignment ya Kingereza na baadhi ya wanafunzi hawakufanya akiwepo Sebastian, Wakati Mwl yupo darasani alimpiga kofi kijana Sebastian na kijana akahoji kwanini anampiga wakashikana koo, ndio walimu wakamchukua na kumpeleka staff room na kuanza kumpiga vile. Tangu tar 29. September mwanafunzi hakuonekana shuleni. Na mwl Esther Harembo wa Iringa University ndio aliyekuwa akisema mwacheni mtamuumiza na ndie aliyechukua video. Hao walimu wote hawapo wameondoka kwenda kwenye vyuo vyao. 

POLISI wanaendelea kuwahoji uongozi wa Mbeya Day Sec School na Mwanafunzi aliyeumizwa ikiwepo kumpeleka hospitali.Nimeelekeza vyombo vya dola Dar wawatafute chuoni kwao hao walimu kuhusiana na shambulio hilo kwa mwanafunzi huyo. 


MWIGULU Nchemba, W MNN

Asante sana @mwigulunchemba kwa kuchukua hatua za haraka! Hii iwe fundisho kwa wengine wanaonyanyasa watoto! #tuwalindewatotowetu

Related

Hot Stories 1864636645362201733

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item