Gawio la wanahisa wa TBL Group laongezeka | LUKAZA BLOG

Gawio la wanahisa wa TBL Group laongezeka

  Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa TBL Group Roberto Jarrin (kushoto) akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TBL Group,W...

 Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa TBL Group Roberto Jarrin (kushoto) akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TBL Group,Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa David Msuya,  wakati wa  mkutano Mkuu wa 43 wa wanahisa uliofanyika   kwenye  Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere  jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa TBL Group Roberto Jarrin, (wapili kutoka kushoto)akifafanua jambo  wakati wa  mkutano Mkuu wa 43 wa wanahisa uliofanyika   kwenye  Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere  jijini Dar es Salaam ,kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TBL Group,Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa David Msuya.Kushoto ni Mkurugenzi wa fedha wa TBL Group Wayne Hall na kulia ni Katibu wa TBL Group Huruma Ntahena.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TBL Group,Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa David Msuya,   (katikati) Mkurugenzi mkuu mtendaji wa TBL Group Roberto Jarrin,(kushoto)  na Katibu wa TBL Group Huruma Ntahena (kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa bodi yawanahisa wa TBL Group wakati wa Mkutano wa 43 wa wanahisa uliofanyika   kwenye  Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere  jijini Dar es Salaam.
 Mmoja wa wajumbe wa  mkutano mkuu wa 43 wa wanahisa  wa TBL Group uliofanyika   kwenye  Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere  jijini Dar es Salaam,akiuliza swali kwenye mkutano huo.
 Wajumbe wa mkutano wa mkutano mkuu wa 43 wa wanahisa  wa TBL Group uliofanyika  kwenye  Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam,wakiwa wamenyosha mikono kuashiria kupitisha ajenda za mkutano huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TBL Group,Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa David Msuya,   (wapili kulia )akisisitiza jambo wakati wa  mkutano Mkuu wa 43 wa wanahisa uliofanyika  leo kwenye  Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere  jijini Dar es Salaam.kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa TBL Group Roberto Jarrin, wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa fedha wa TBL Group Wayne Hall na kulia ni Katibu  wa TBL Group Huruma Ntahena.

Mkutano mkuu wa 43 wa mwaka wa wanahisa wa TBL Group umefanyika jijini Dar es  Salaam ambapo Mwenyekiti wa bodi wa kampuni hiyo,Mh.Cleopa David Msuya alielezea mafanikio mbalimbali ambayo kampuni inaendelea kuyapata.

Moja ya mafanikio ambayo ameyabainisha ni kupatikana kwa faida ya shilingi bilioni 331 katika mwaka uliopita wa fedha ambapo ni ongezeko la asilimia 4%  ya mauzo kulinganisha na mwaka uliotangulia na ongezeko hilo limepelekea kupanda kwa gawio la  wanahisa kufikia shilingi 600/-kwa hisa.
Mh.Msuya,alisema kuwa na changamoto mbalimbali za kiuchumi zilizopo nchini kampuni imeendelea kutoa mchango mkubwa serikalini kupitia kodi ya mapato,ushuru na kodi  ya ongezeko la thamani ambapo imelipa bilioni 475 na kuendelea kutambuliwa na Mamlaka ya Mapato kuwa miongoni mwa wachangiaji wakubwa wa mapato ya serikali.
 
Alisema katika kipindi cha mwaka huu kampuni itaendelea kufanya jitihada za kuongeza uzalishaji na mauzo ikiwemo kusaidia huduma mbalimbali za kijamii  ikiwemo kukuza sekta ya kilimo nchini kupitia viwanda.

Related

Biashara 5013053090535229003

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item