Mwanamke Wa Wakati Ujao: Njia ya kuwapeleka Wanawake kushika nafasi za Uongozi | LUKAZA BLOG

Mwanamke Wa Wakati Ujao: Njia ya kuwapeleka Wanawake kushika nafasi za Uongozi

Warda akichapa kaza katika ofisi za TDL jijini Dar es Salaam “ Elimu ni ufunguo wa maisha na    kumpatia elimu mwanamke ni kuelimisha...

Warda akichapa kaza katika ofisi za TDL jijini Dar es Salaam

Elimu ni ufunguo wa maisha na  kumpatia elimu mwanamke ni kuelimisha taifa zima.Pamoja na ukweli wa msemo huu wanawake wengi hususani katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania bado wamebaki nyuma kielimu ikiwemo kupatiwa nafasi za uongozi zenye kutoa maamuzi”.Anasema Warda Kimaro,Meneja Chapa (Brand Manager) wa vinywaji wa kampuni ya Tanzania Distillers Limited (TDL),kampuni tanzu ya TBL Group.
 
 Kuondokana  na changamoto ya kubaki nyuma anashauri wanawake  kupambana kusoma kwa bidii na wanapopata fursa kuzitumia vizuri ili kuondoa dhana kuwa wanawake hawana uwezo au wanahitaji upendeleo maalumu katika  kushika nafasi mbalimbali za kazi ama uongozi.
Katika mahojiano hivi karibuni Warda Kimaro, alisema kuwa anajivunia kuajiriwa na kampuni kubwa kama TDL ambapo amepatiwa nafasi inayomuwezesha kutoa maamuzi na amekuwa akitoa mawazo mbalimbali na yamekuwa yakiheshimiwa bila kujali jinsia yake na umri wake.
 
Akiwa  ni msomi mwenye taaluma ya Masoko kutoka Chuo Kikuu cha Southhampton Solent kilichopo  nchini  Uingereza na mwanafunzi wa  mwaka wa mwisho wa shahada ya uzamili katika Utawala  na Uendeshaji Biashara (MBA) kutoka chuo cha ESAMI anasema  kwa sasa  ni miongoni mwa wanafunzi wanaopata mafunzo ya kumjengea mwanamke nafasi ya kiutawala katika progamu inaojulikana kama ‘Mwanamke Wa Wakati Ujao’ au kitaalamu kama Female Future Progamme.
 
 Alisema mafunzo haya yanayotolewa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa kushirikiana na taasisi ya Confederation of Norwegian Enterprises katika taasisi ya ESAMI  ni ya aina yake kwa kuwa yanawezesha kupata maarifa ya masuala mbalimbali hususani utawala  na jinsi ya kushiriki na kutoa mawazo kwenye vikao vya bodi.
 
Aliongeza kuwa Programu za aina hii ni nzuri hususani kwa wanawake kwa kuwa mafunzo yanayotolewa yanaongeza uwezo wa kujiamini   na kuna haja ya kuwa na programu nyingi za aina hii ili ziwafikie wanawake wengi popote walipo nchini.
 
“Ili wanawake wengi kutobaki nyuma silaha pekee ya kuwakwamua ni elimu na ninaposema elimu simaanishi kupata  shahada za juu bali ni kujifunza mambo mbalimbali na kupata maarifa na kuungana na kushirikiana  ambapo watapata fursa ya kubadilishana uzoefu wa masuala mbalimbali,kupeana moyo na kupanga mikakati ya kutatua changamoto zinazowakabili”.Alisema.
 
Aliishukuru kampuni ya TDL kwa kumpatia fursa ya kupata mafunzo haya na anavutiwa mkakati wa kampuni hiyo kupitia programu yake ya TBL Women’s Forum (TWF) kwa kuwapatia nafasi za uongozi wanawake katika vitengo mbalimbali ambapo wanaendelea kufanya vizuri na kudhihirisha kuwa ujuzi hauna jinsia.
 
 “Najua zipo changamoto nyingi zinatukabili kama wanawake lakini vichwani mwetu tuondoe dhana kuwa tunapaswa kuwa nyuma ya wanaume kwa kila jambo,tukiondokana na dhana hiyo tutaweza kusonga mbele na ipo mifano ya wanawake hapa nchini wanaendelea kung’ara katika nafasi zao za kazi kuzidi hata wanaume na kufanya kwao vizuri kunatokana na elimu walionayo na kujiamini”.Alisisitiza.
 
Akiongea juu ya Progamu hii,Bi.Lilian Machera kutoka Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) ambaye anairatibu alisema hii ni programu   ambayo dhumuni lake ni kuwajengea uwezo wanawake kushika nafasi za uongozi. “Utafiti tuliofanya  umebainisha kuwa ni wanawake asilimia 35% ndio wanashikilia nafasi za uongozi wakati wanaume wanashikilia asilimia 65%.
 
Alisema mtaala wa mafunzo haya umejikiza zaidi katika masuala ya utawala,jinsi ya kutoa michango ya mawazo kwa ufasaha kwenye vikao vya juu vya bodi za makampuni,kuongea mbele ya watu kwa ufasaha,kujiamini katika kazi na kwenye kutoa maamuzi sahihi,jinsi ya kujenga hoja sahihi kwenye vikao,uchambuzi wa ripoti mbalimbali kwa haraka na mengineyo mengi.
 
Mratibu mwenza wa Programu hii kutoka taasisi ya Confederation of Norwegian Enterprises (NHO), Ms Mavie Bordvik, amesema mpango wa mafunzo haya tayari umenufaisha wanawake zaidi ya 200 katika nchi ulipoanzia zikiwemo nchi za Nigeria,Kenya na Uganda.
 

Alitoa wito kwa wanawake wote wa Tanzania kuamka na kuchangamkia fursa za kujiendeleza zinapojitokeza na kuachana na mawazo ya kujiona wanyonge mbele ya wanaume.

Related

Biashara 8386223029006744259

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item