Scopion Afutiwa Mashitaka na Mahakama ya Ilala | LUKAZA BLOG

Scopion Afutiwa Mashitaka na Mahakama ya Ilala

Taarifa tulizozipata kutoka Mahakama ya Ilala Jijini Dar Es Salaam, zinasema kuwa Kijana anayetuhumiwa kumtoboa macho Said ajulikanae kwa...

Taarifa tulizozipata kutoka Mahakama ya Ilala Jijini Dar Es Salaam, zinasema kuwa Kijana anayetuhumiwa kumtoboa macho Said ajulikanae kwa jina la Scopion Amefutiwa  shitaka la unyang’anyi kwa kutumia silaha lililokuwa likimkabili.

Taarifa zinasema kuwa Upande wa mashtaka umeomba shitaka hilo liondolewe mahakamani kwasababu hawana nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Unaweza pata taarifa kamili iliyoandikwa na Khadija Jumanne wa Gazeti la Mwananchi Kama inavyosomeka hapo chini

Na Khadija Jumanne, Mwananchi


Dar Es Salaam. Mahakama ya Wilaya ya Ilala, imemfutia shtaka linalomkabili mshtakiwa Salumu Njwete baada ya upande wa mashtaka kuomba shtaka hilo liondolewe mahakamani kwa sababu hawana nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Kutokana na maombi hayo, Hakimu Adelf Sachore amekubaliana na ombi hilo kwa kuzingatia kifungu namba 91 kifungu kidogo cha kwanza cha sheria ambacho kinampa Mamlaka Mkurugenzi Wa Mashtaka nchini (DPP) kuondoa shtaka mahakamani muda wowote ili mradi kama kesi hiyo haijatolewa hukumu.

Lakini kifungu hicho kinampa Mamlaka DPP kumshtaki mshtakiwa huyo endapo kama ana nia ya kuendesha shtaka hilo.

Njwete anakabiliwa na shtaka la unyang'anyi wa kutumia silaha na kumjeruhi Saidi Mrisho. Lakini shtaka hili limefutwa hata hivyo anaweza kufunguliwa shtaka lingine.Chanzo Mwananchi Online

Related

Hot Stories 6605958992050655373

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item