TBL Group yaadhimisha mwezi wa Saratani ya matiti kwa vitendo | LUKAZA BLOG

TBL Group yaadhimisha mwezi wa Saratani ya matiti kwa vitendo

  - Yaendesha zoezi la kupima afya za wafanyakazi na familia zao   Wafanyakazi wa kampuni ya    TBL Group katika viwanda vyake vyot...


 
-Yaendesha zoezi la kupima afya za wafanyakazi na familia zao
 
Wafanyakazi wa kampuni ya  TBL Group katika viwanda vyake vyote nchini vilivyopo katika mikoa ya Dar Es Salaam,Mwanza,Mbeya,Arusha na Kilimanjaro mwishoni mwa wiki walipimwa Saratani ya matiti ikiwemo kupatiwa elimu juu ya ugonjwa huu ambao umekuwa ukiongezeka kwa kasi nchini ikiwa ni maadhimisho ya Mwezi wa Saratani ya Matiti kupitia mpango wa kampuni wa Afya Kwanza.
 
 Meneja  Raslimali watu wa kampuni hiyo,Bw.Jonathan Koshuma,amesema kuwa zoezi hili limetekelezwa nchini ya Mpango wa kuimarisha afya za wafanyakazi pamoja na familia zao unaojulikana kama Afya Kwanza ikiwa pia ni kuadhimisha mwezi wa Saratani ya matiti kwa vitendo.

Koshuma amesema  tangu mpango huu uanze kutekelezwa na kampuni umeanza kuonyesha mafanikio makubwa kwa kuwa wafanyakazi wanapata fursa ya  kupata elimu ya afya ya kujikinga na magonjwa mbalimbali  elimu ambayo pia inatolewa wa familia za wafanyakazi.

“Mwitikio wa wafanyakazi wetu wote kushiriki katika programu hii ni mzuri kama ambavyo wengi wamejitokeza kupimwa na kupatiwa ushauri wa jinsi ya kuepuka ugonjwa wa Saratani ya Matiti na kujua dalili za ugonjwa huu mapema pindi unapojitokeza ili kuwahi kufanyiwa uchunguzi na kupata matibabu”.Alisema Koshuma.

 Alisema mbali na kampuni kuwa na utaratibu mzuri wa kuhakikisha wafanyakazi wake na familia zao wana bima ya afya na kuwa na zahanati katika viwanda vyake bado imeonelea kuna umuhimu wa kuhakikisha wanapata elimu ya kinga kwa kuwa kinga ni bora kuliko matibabu.


 Mratibu wa Programu ya Afya Kwanza wa TBL Group,Julieth Mgani amesema kuwa mbali na wafanyakazi kupatiwa elimu na ushauri nasaha kuhusiana na magonjwa mbalimbali pia wanapata fursa ya kushiriki kufanya mazoezi ya pamoja yanayoshirikisha pia familia zao pia wamekuwa wakipatiwa elimu kuhusiana na masuala ya umuhimu wa lishe bora.
 -Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Arusha wakiwa kwenye semina ya Saratani ya matiti ambapo pia walipata fursa ya kuuliza maswali mbalimbali kusiana na ugonjwa huo
 Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Dar wakifuatilia mafunzo kuhusiana na saratani ya matiti
 Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Mbeya wakifuatilia mafunzo kuhusiana na Saratani ya matiti
Wafanyakazi wa TBL Mwanza wakipima afya zao

Related

Kijamii 6065745862942700088

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item