Wafanyakazi wa TBL Group walivyoshiriki kampeni ya ‘Mti Wangu’ | LUKAZA BLOG

Wafanyakazi wa TBL Group walivyoshiriki kampeni ya ‘Mti Wangu’

Katika kutekeleza mkakati wa kampuni wa kutunza mazingira na sera ya wafanyakazi kutumia muda wao kwa ajili ya kazi za kijamii,baadhi ya wa...

Katika kutekeleza mkakati wa kampuni wa kutunza mazingira na sera ya wafanyakazi kutumia muda wao kwa ajili ya kazi za kijamii,baadhi ya wafanyakazi wa TBL Group wameungana na viongozi wa serikali na wafanyakazi wa taasisi mbalimbali za kiserikali na za binafsi katika kampeni ya uhamasishaji upandaji miti inaojulikana kama Mti Wangu.
Kampeni hii imezinduliwa leo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh.Samia Suluhu Hassan katika eneo la viwanja vya Gymkhana.
Wafanyakazi wa TBL Group  wakiongozwa na Meneja wa Afya na Usalama Renatus Nyanda na Meneja Ufanisi Wa Uzalishaji  Charles Nkondola wakishiriki kupanda mti katika viwanja vya Gymkhana eneo la barabara  ya Barack Obama ikiwa ni uzinduzi wa  kampeni ya ‘Mti Wangu’ iliyozinduliwa na Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan    
Diwani wa kata ya Kivukoni manispaa ya Ilala Henry Massaba wa pili (kushoto)  akimkabdhi mti wa kupanda  Meneja Ufanisi wa Uzalishaji Charles Nkondola Charles Nkondola  kwa niaba waya wafanyakazi wa TBL Group wakati wa uzinduzi wa  kampeni ya ‘Mti Wangu’ .Kushoto ni Meneja wa Afya na USalama, Renatus Nyanda.
Meneja wa Ufanisi wa Uzalishaji wa TBL Group Charles Nkondola akibadilishana mawazo na   Afisa Mazingira wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam,Estha Masomba wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti kwenye viwanja vya Gymkhana .kushoto ni Meneja wa Afya na Salama Renatus Nyanda.
Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema  (kushoto)akisalimiana na  Meneja wa Ufanisi wa Uzalishaji wa TBL Group Charles Nkondola, mara baada ya kumaliza zoezi la upandaji miti  eneo la Gymkhana.
Wafanyakazi wa TBL Group wakishiriki katika zoezi la upandaji miti 

Related

kitaifa 5223366674848838355

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item