WANAHABARI WAPIGWA MSASA KUHUSU KINGATIBA YA MABUSHA, MATENDE, USUBI, KICHOCHO, TRAKOMA | LUKAZA BLOG

WANAHABARI WAPIGWA MSASA KUHUSU KINGATIBA YA MABUSHA, MATENDE, USUBI, KICHOCHO, TRAKOMA

 Ofisa Mradi wa Mpango wa Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele, Oscar Kaitaba akielezea umuhimu wa vyombo vya habari kuelimisha umma ...

 Ofisa Mradi wa Mpango wa Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele, Oscar Kaitaba akielezea umuhimu wa vyombo vya habari kuelimisha umma kujenga tabia ya  kutumia Kingatiba ya magonjwa ya kichocho, Minyoo ya Tumbo, Usubi Matende na Mabusha wakati wa Warsha iliyoshirikisha wanahabari, Dar es Salaam leo. Kampeni ya kuwapatia wananchi Tibakinga kwa wakazi takribani mil. 4 wa Jiji la Dar es Salaam itaanza Oktoba 25 waka huu. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

 Meneja Mradi wa Mpango wa Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele, Upendo Mwingira akifafanua jambo wakati wa warsha hiyo.

 Wanahabari wakiwa katika warsha hiyo Mtangazaji wa BBC, Halima Kassim akitafakari jambo  kuhusu semina hiyo ya wanahabari kupata uelewa kuhusu magonjwa hayo na jinsi ya kuwaelimisha wananchi kutumia Kingatiba kwa kumeza  dawa mara noja kila mwaka ili kuboresha afya Mtaalamu Kaitaba akionesha baadhi ya dawa za Kingatiba ya magonjwa hayo Ofisa Habari wa Mradi huo, Said Makora akiwataka wanahabari kuwaelimiasha wananchi juu ya magonjwa hayo na jinsi ya kupata Kingatiba kwa kuandika makala, habari, majarida na kutumia mitandao ya kijamii kwa nia ya kuyatokomeza magonjwa hayo kufikia mwaka 2020.

 Kaitaba akionesha vifaa vinavyotumika kuwapima watu ili wapewe dawa kulingana na kimo chake.

 Mwandishi wa Habari wa Nipashe, Jasmin akichangia mada wakati wa semina hiyo.

 Wana habari wakipatiwa dawa za Kingatiba za magonjwa hayoMtangazaji wa E FM Radio akipimwa urefu ndipo apatiwe dawa 

Related

kitaifa 5519825294691991482

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item