Watumiaji wengi wa kinywaji cha Chibuku wakiri ni bia ya asili ya kitanzania | LUKAZA BLOG

Watumiaji wengi wa kinywaji cha Chibuku wakiri ni bia ya asili ya kitanzania

  Wateja wakifurahia bia ya Chibuku katika moja ya promosheni ya 5 Star jijini Dar es Salaam   Baadhi ya watumiaji wa bia ya Chibuk...

 Wateja wakifurahia bia ya Chibuku katika moja ya promosheni ya 5 Star jijini Dar es Salaam
 Baadhi ya watumiaji wa bia ya Chibuku wakimsikiliza Afisa Mauzo wa Darbrew (kulia) alipokuwa akiwaeleza faida za kutumia kinywaji hiki
Mteja wa bia ya Chibuku akipokea kipeperushi chenye maelezo ya kampeni ya 5 Star kutoka kwa mmoja wa Maafisa Mauzo wa  Darbrew wakati wa moja ya promosheni jijini Dar es Salaam
-Promosheni ya Five Star yazidi kushika kasi
Watumiaji wengi wa bia ya asili ya Chibuku inayotengenezwa na kampuni ya DarBrew jijini Dar es Salaam wamesema kuwa kinywaji hiki ni bia ya asili ya kitanzania kwa kuwa kina vionjo vya pombe mbalimbali za asili kutoka makabila mbalimbali ya Tanzania.
Wamesema kuwa tofauti ya bia ya Chibuku na pombe hizo ni kwamba imetengenezwa katika mazingira salama na inamfikia mtumiaji ikiwa imefungwa kwenye vifaa  bora na katika mazingira ya usafi.
Bwana Simon Mkude,mkazi wa Buguruni akiongea kwa niaba ya wenzake amesema kuwa hivi sasa watumiaji wengi wa pombe za asili wamegundua ubora wa bia ya Chibuku na wameanza kuachana na pombe za asili ambazo hazina viwango na zinauzwa katika mazingira yasiyo salama kwa afya.
Aletas Matabila mkazi wa Mbezi anasema kuwa yeye na wenzake hivi sasa wameamua kutumia bia ya Chibuku kwa kuwa licha ya unafuu wa bei inapatikana kwa gharama nafuu na haivurugi bajeti kama vilivyo vinywaji vingine ambavyo vinapatikana kwa bei ya juu.
Maria Lous mkazi wa Kibamba akiongea kwa niaba ya wenzake katika baa ya Mbezi Inn alisema bia ya Chibuku ni salama kiafya na ina lishe tofauti na vinywaji vingine ambavyo vinadhoofisha afya za watumiaji wake.
Wakati wananchi wanaendelea kufurahia ubora wa bia ya Chibuku kampuni inaendelea na promosheni ya Five Stars ambayo imelenga  kuwezesha wananchi wengi kuelewa ubora wake na kwa jinsi gani kinaleta burudani sambamba na kupunguza gharama za maisha
 Jina la Five Star au Nyota Tano kwa Kiswahili katika kampeni hii ambapo kila nyota inaeleza hali halisia wa bia hii ya asili na ubora wake katika kuitumia.
 Nyota ya kwanza inaelezea kuwa Bia ya asili ya Chibuku ni Bia ya asili ya Kiafrika kutokana na jinsi inavyokubalika katika nchi mbalimbali za Afrika  kwa kutumiwa na wengi kama kiburudisho baada ya saa za kazi.
 Nyota ya pili inaelezea vionjo vyenye kiwango cha juu vya bia ya Chibuku vinavyotokana na mchanganyiko wa malighafi za nafaka zinazotumika kutengenezea kinywaji hiki
 Nyota ya tatu inaelezea radha inayoridhisha ya bia ya Chibuku   ambayo inapendeza mdomoni na kuleta raha na burudani ya aina yake.
 Nyota ya nne inaelezea ubora wa hali ya juu wa bia ya asili ya Chibuku  kutokana na kutengenezwa kitaalamu na kuwa na viwango vinavyotakiwa vya ubora usioleta madhara kwa mtumiaji
Nyota ya tano inaelezea kuwa bia ya Chibuku ni kwa ajili yetu sote kutokana na ubora wake inaweza kutumiwa na watu wenye mitindo ya maisha ya aina mbalimbali pia inapatikana kwenye chupa zenye ujazo wa aina mbalimbali,hali ambayo inawezesha mtumiaji kukipata kinywaji hiki kulingana na mfuko wake ulivyo.

Kampeni  ya Five Stars inaendelea kufanyika kwenye vilabu  na sehemu nyingi inapouzwa bia ya Chibuku Super na inazidi kuwafikia wengi na watumiaji wake kuongezeka , wengi mbali na kuvutiwa na radha nzuri ya bia hii  ya asili wanavutiwa kwa jinsi ilivyofungwa na inavyowafikia watumiaji ikiwa katika mazingira ya usafi na wengi wanakiri  kuwa Chibuku ni bia  ya asili ya kitanzania inayolinda  afya za watumiaji wake na kurahisisha maisha

Related

Biashara 8226746046470232106

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item