BODI YA FILAMU NCHINI YAWATOA GIZANI ZAIDI YA WASANII 300 WA FILAMU MKOANI MWANZA. | LUKAZA BLOG

BODI YA FILAMU NCHINI YAWATOA GIZANI ZAIDI YA WASANII 300 WA FILAMU MKOANI MWANZA.

Zaidi ya wasanii 300 wa filamu mkoani Mwanza, jana wakifuatilia mafunzo kuhusu weledi wa sanaa ya filamu kutoka kwa mkufunzi, Richard Ndu...

Zaidi ya wasanii 300 wa filamu mkoani Mwanza, jana wakifuatilia mafunzo kuhusu weledi wa sanaa ya filamu kutoka kwa mkufunzi, Richard Ndunguru, wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

Mafunzo hayo ni ya siku tatu ambapo yameandaliwa bure na Bodi ya Filamu nchini, yalianza juzi Novemba 10 na yatafikia tamati leo Novemba 12,2016 ambapo washiriki watakabidhiwa vyeti na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella.

Wasanii, waongozaji pamoja na waandishi wa filamu wamepatiwa mafunzo hayo ili kuboresha kazi zao ikiwemo kuzingatia kazi zenye maadili na maudhui ya mtanzania na zaidi kutambua haki zao ikiwemo hakimiliki za kazi zao na namna ya kuuza kaziuza kwa faida.
Na BMG
Mkufunzi, Richard Ndunguru, kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam, akiwasilisha mada jana kwenye mafunzo ya sanaa ya filamu mkoani Mwanza.
Washiriki wa mafunzo ya sanaa ya filamu mkoani Mwanza
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wameishukuru Serikali kupitia Bodi ya Filamu nchini kwa kuwafikishia mafunzo hayo bure na kwamba yatawasaida kuboresha kazi zao na kulifanya soko la filamu mkoani Mwanza kukua.

Related

Filamu 3928046633040546105

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item