KABAGO, MKONGWE KWENYE MUZIKI WA KUCHANA NCHINI KUACHIA WIMBO MPYA. | LUKAZA BLOG

KABAGO, MKONGWE KWENYE MUZIKI WA KUCHANA NCHINI KUACHIA WIMBO MPYA.

Kupitia vyombo mbalimbali vya redio, kesho jumatano Novemba 09, 2016 mkongwe wa muziki wa kuchana nchini, Filbert Kabago "Kabago&quo...

Kupitia vyombo mbalimbali vya redio, kesho jumatano Novemba 09, 2016 mkongwe wa muziki wa kuchana nchini, Filbert Kabago "Kabago", ataachia wimbo wake mpya uitwao Tanzania akiwa amemshirikisha Hadmad.

Kabago anatambulika kama mmoja wa watu waliowezesha hiphop nchini kusonga mbele tangu akiwa mkoani Arusha na hata alipohamia Mwanza, akiwa kama msanii na mtangazaji wa redio (kwa sasa Passion Fm Mwanza).

Atakumbukwa namna alivyosaidia kwenye harakati za kimaendeleo Jijini Mwanza kupitia kazi zake za muziki na hata namna wimbo wa tatizo la umeme ulivyoleta nafuu kwa wakazi wa Jiji la Mwanza.

Kama hiyo haitoshi, mchango wake redioni ni mkubwa kwa wasanii mbalimbali hususani wanaochipukia ambapo wengi wao ambao sasa ni wanavuma akiwemo Baraka Da Prince na Young Killer, wamepitia mikononi mwake. 

Kaa tayari kuusubiri wimbo wa Kabago uitwao Tanzania ambao umetengenezwa kwenye studio yake iitwayo K-Records chini ya produza Sam Music.

Related

Burudani 8821840247730755239

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item