TBL Group yashiriki kampeni ya kuondoa tatizo la madawati mashuleni nchini | LUKAZA BLOG

TBL Group yashiriki kampeni ya kuondoa tatizo la madawati mashuleni nchini

  Katika mkakati wake wa kuondoa kero kwenye jamii katika sekta mbalimbali,kampuni ya TBL Group imeshiriki kudhamini harambee ya kuchangish...

 Katika mkakati wake wa kuondoa kero kwenye jamii katika sekta mbalimbali,kampuni ya TBL Group imeshiriki kudhamini harambee ya kuchangisha fedha kwa aijli ya ununuzi wa madawati pamoja na uboreshaji elimu nchini iliyoandaliwa na  taasisi ya Hassan Majaar Tust na kufanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri Mkuu ,Mh.Kassim Majaliwa.
 
Mbali na kampuni kutoa udhamini baadhi ya wafanyakazi walishiriki katika harambee hiyo na waliguswa na tatizo la changamoto za mazingira ya kusomea nchini ambapo walijitoa pia kuchangia kuondoa tatizo hili.
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Group wakiwa katika picha ya pamoja na  Waziri Mkuu,Mh.  Kassim Majaliwa, watatu (katikati) Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Bank M,Jacqueline Woisso na Mtendaji Mkuu wa Hassan Maajar Trust Balozi Bertha Semu,Meneja rasmali watu wa TBL Group Lilian Makau, Afisa Uhusiano wa TBL Group, Editha Mushi  (wa pili kulia) na Mwenyekiti wa Hassan Maajar Trust,Balozi Mwanaidi Maajar wakati wa harambee ya kuchangia fedha kwa ajili ya ununuzi wa madawati pamoja na  uboreshaji wa shule nchini, iliyoandaliwa na mfuko wa Wakfu wa Hassan Maajar (Hassan Maajar Trust) jijini Dar es Salaam ambapo TBL ilikuwa mmoja wa wadhamini.

Waziri Mkuu,Mh.  Kassim Majaliwa watatu (kushoto) akisalimiana na  Afisa Uhusiano wa TBL Group, Editha Mushi, wakati wa harambee ya kuchangia fedha kwa ajili ya ununuzi wa madawati pamoja na  uboreshaji wa shule nchini, iliyoandaliwa na mfuko wa Wakfu wa Hassan Maajar (Hassan Maajar Trust) na kufanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee  jijini Dar es Salaam .Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Bank M,Jacqueline Woisso na Mtendaji Mkuu wa Hassan Maajar Trust, Balozi Bertha Semu.TBL Group ilikuwa mmoja wa wadhamini wa harambee hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Group wakisikiliza hutuba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (hayupo pichani) wakati wa harambee hiyo

Wafanyakazi wa TBL Group kitengo cha Uhusiano wakiwa katika picha pamoja mara baada ya kuchangia fedha kwa ajili ya  ununuzi wa madawati pomoja na uboreshaji wa shule nchini
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Group wakijaza fomu za kuchangia fedha kwa ajili ya ununuzi wa madawati pamoja na uboreshaji wa shule nchini wakati wa harambee hiyo.

Related

Kijamii 4581866420172460645

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item