BASI LA KANDAHAR LAGONGA LAUA ARUSHA | LUKAZA BLOG

BASI LA KANDAHAR LAGONGA LAUA ARUSHA

Basi l a Kampuni  ya  Kandahar kama linavyoonekana  pich ani( P icha pamoja na  habari  na  Vero Ignatus Blog) Na.Vero  Ignatus Arus...

Displaying IMG_5329.JPG
Basi la Kampuni ya  Kandahar kama linavyoonekana  pichani( Picha pamoja na habari  na  Vero Ignatus Blog)

Na.Vero Ignatus Arusha.

Basi la kampuni ya Kandahari T 785 DFM limemgonga mtembea kwa miguu na kusababisha kifo chake papo hapo.

Akizungumzia mazingira ya ajali hiyo Kamanda wa polisi mkoani Arusha Charles Mkumbo amesema ajali hiyo imetokea leo majira ya saa sita na nusu mchana Jijini hapa.

Amesema  kuwa basi hilo lilikuwa linatokea Moshi kuelekea singida lakini lilipofika Arusha kwenye kivuko cha watembea kwa miguu chini ya mti ( zebra crossing ) dereva alikaidi kusimama ili watembea kwa miguu wavuke ndipo aliposabababisha kifo cha mtoto huyo.

"Dereva huyo alifika zebra crossing hakusimama kuna mama alikuwa anavuka  pamoja na mwanae, mama yeye alifanikiwa kukimbia lakini mtoto aligongwa na kufariki papo hapo"alisema kamanda. 

Aidha amemtaja dereva aliyekuwa anaendesha basi hilo kuwa ni Immanuel Nyari miaka( 46) mkazi wa mbauda jijini hapa ,pamoja na jina la marehemu ni Ezra Samson miaka (7) mkazi wa Sombetini.

Kamanda Charles Mkumbo amewataka madereva waheshimu na kuzingatia sheria za usalama barabarani ikiwemo kwenye vivuko,madaraja,kwenye kona huku wakitambua kuwa hawatumii barabara peke yao.


Amesema madereva ambao watakiuka kuheshimu na kuzingatia sheria za usalama barabarani watawachukulia hatua kali za kisheria pamoja na kuwanyang'anya leseni  

Related

kitaifa 9164585315519716628

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item