TBL Group yang’ara tuzo ya NBAA | LUKAZA BLOG

TBL Group yang’ara tuzo ya NBAA

-Ni kutokana na utunzaji mzuri wa hesabu za fedha   Kampuni ya TBL Group imezidi kung’ara katika tuzo ya utunzaji wa mahesabu na uwasil...

-Ni kutokana na utunzaji mzuri wa hesabu za fedha
 
Kampuni ya TBL Group imezidi kung’ara katika tuzo ya utunzaji wa mahesabu na uwasilishaji wa taarifa za fedha katika shindano  linalotayarishwa na Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa mahesabu (NBAA) kila mwaka na kuhusisha taasisi za serikali na makampuni binafsi katika sekta mbalimbali.
Mwaka huu TBL Group imeshika nafasi ya pili katika sekta ya viwanda vikubwa ambapo mwaka jana  iliongoza na kutunukiwa tuzo ya ushindi wa jumla  wa shindano hilo.
Akiongea muda mfupi baada ya kutunikiwa tuzo katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaamya uwakilishaji  ,Mhasibu mwandamizi  kutoka TBL Group, Alois Qande, alisema   kuwa  kampuni hiyo itaendelea kuwa mfano wa uwekezaji wenye tija na itaendelea kufanya vizuri katika nyanja mbalimbali ikiwemo kuweka kipaumbele katika kuchangia pato la taifa kwa kulipa kodi kwa wakati mwafaka.
 
“Tuzo kama hizi kwetu TBL Group tunazithamini sana kwa kuwa  zinaleta motisha kwetu na kufanya kampuni itambulike kitaifa na kimataifa na natoa wito kwa watanzania wote kununua na kuzitumia bidhaa zinazozalishwa na  makampuni ya hapa nchini kwa kuwa ndizo zinasababisha nchi kukua kiuchumi na kuondokana na umaskini”.Alisema.
 
Amesema kampuni imejipanga kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi wenye viwango ili kukuza sekta ya viwanda nchini na kuongeza fursa za ajira kwa watanzania “Kupitia biashara ya kampuni idadi kubwa ya watanzania wanaendelea kunufaika kupitia ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja”.Alisema
 
 
 Mameneja wa Vitengo cha Uhasibu wa TBL Group kutoka kushoto, Alois Qande  na Edward Peter wakifurahia tuzo ya ushindi.
 Mhasibu Mwandamizi wa TBL Group, Alois Qande akipokea tuzo kwa niaba ya kampuni kutoka kwa Kamshna Shogholo Msangi.
 Mkurugenzi Mtendaji wa bodi ya Uhasibu na ukaguguzi wa mahesabu nchin (NBAA)  Pius Maneno akimpongeza mfanyakazi wa TBL Group Alois Qande mara baada ya kuibuka mshindi wa Tuzo ya utunzaji bora wa mahesabu wa mwaka 2015 wakati wa hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Wengine kwenye picha wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa bodi hiyo Profesa Isaya Jairo na Kamishna Shogholo Msangi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango.
 Mkurugenzi Mtendaji wa bodi ya Uhasibu na ukaguguzi wa mahesabu nchin (NBAA)  Pius Maneno akimpongeza mfanyakazi wa TBL Group Alois Qande mara baada ya kuibuka mshindi wa Tuzo ya utunzaji bora wa mahesabu wa mwaka 2015 wakati wa hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Wengine kwenye picha wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa bodi hiyo Profesa Isaya Jairo na Kamishna Shogholo Msangi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango.
Wafanyakazi wa TBL Group wakiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wengine kutoka makampuni mbalimbali

Related

kitaifa 2812724781806405471

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item