Balozi Mgaza apigia chapuo ‘Hapa Kazi Tu’ Saudi Arabia | LUKAZA BLOG

Balozi Mgaza apigia chapuo ‘Hapa Kazi Tu’ Saudi Arabia

Na Mwandishi Maalum,  Saudi Arabia WATANZANIA waishio  nchini Saudi Arabia, wametakiwa kufanya juhudi za kuitangaza nchi yao pamo...


Na Mwandishi Maalum, Saudi Arabia

WATANZANIA waishio 
nchini Saudi Arabia, wametakiwa kufanya juhudi za kuitangaza nchi yao pamoja na 
kuangalia namna ya kutekeleza kiu ya nchi ya viwanda kama ilivyoasisiwa na Rais 
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dr John Pombe Magufuli.
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemedi Mgaza, mwenye suti nyeusi, akifurahia jambo ofisini kwa Waziri anayeshughulikia Masuala ya Hijja na Umrah wa Serikali ya Saudi Arabia, Mhe. Dr. Mohammed Saleh Bin Taher Benten, alipofika ofisini kwake kujadiliana mambo mbalimbali ikiwamo hija ya mwaka huu wa 2017.

Baadhi ya Watanzania wanaoishi nchini Saudi Arabia, wakimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemedi Mgaza, hayupo pichani walipokutana katika kikao cha pamoja kwa ajili ya kuangalia fursa za kimaendeleo nchini Tanzania.

Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki mjini Jeddah, Saudi Arabia na Balozi wa Tanzania nchini hapa, H.E Hemedi Mgaza, alipofanya kikao na Watanzania waishio nchini hapa kama njia za kushirikiana na wadau hao kwa ajili ya kupeleka maendeleo ya uhakika nchini Tanzania na kuisimamia kwa vitendo kauli mbiu ya ‘Hapa Kazi Tu’.

Akizungumzia juu ya fursa ya uwekezaji nchini Tanzania, Balozi Mgaza alisema ni wajibu wa kila mmoja kufanya kazi kwa nafasi yake kwa ajili ya kukuza uchumi wa nchi yao. Alisema mbali na Watanzania hao kuwekeza kwao kama uwezo wanao, pia wanaweza kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii kwa ajili ya kuchangia fursa hiyo ya watalii inayolipa duniani kote.

Kikao kinaendelea.Kikao kinaendelea. 
“Tukitoka hapa kila  mmoja awe balozi shupavu wa kuitangaza nchi yetu ya Tanzania ili pamoja na  mambo mengine, tuwe tumechangia ukuzaji wa uchumi wetu kulingana na uwezo wetu 
kwa kupitia sekta nyeti ya utalii, ambapo pia kama sehemu ya serikali nilisikiliza maoni na ushauri wao ili tusonge mbele..


“Tuonyeshe mazuri ya 
nchi yetu pamoja na sisi wenyewe kushiriki katika fursa za kiuchumi kuliko 
kusubiri wengine wafanye wakati tunajua fika kuwa kila mmoja ana wajibu wa 
kuiletea maendeleo nchi yetu,” alisema Balozi Mgaza.


Kabla ya kikao hicho na 
Watanzania, Balozi Mgaza pia alifanya mazungumzo na Waziri anayeshughulikia Masuala ya Hijja na Umrah 
wa Serikali ya Saudi Arabia, Mhe. Dr. Mohammed Saleh Bin Taher Benten.


Katika kikao hicho kilichofanyika ofisini kwa waziri huyo, H.E Mgaza alijadiliana na Dr. Benten masuala mbalimbali yanayohusu maandalizi ya ibada ya Hijja ya mwaka 2017 na  fursa kwa mahujaji wa Tanzania.

Related

kitaifa 2913771443683357431

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item