MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MKURUGENZI WA UNEP | LUKAZA BLOG

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MKURUGENZI WA UNEP

  Makamu  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na  Mkurugenzi Mkuu wa UNEP Bw. Erik Solheim ...


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na  Mkurugenzi Mkuu wa UNEP Bw. Erik Solheim ambaye yupo nchini kwa ziara ya siku 2.


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na  Mkurugenzi Mkuu wa UNEP Bw. Erik Solheim ambaye ameongozana na ujumbe wake kwa ziara ya siku 2 wengine waliohudhuria ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Januari Makamba (kulia) na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Faustine Kamuzora.


 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Januari Makamba akifafanua jambo wakati wa mkutano wa  Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  na  Mkurugenzi Mkuu wa UNEP Bw. Erik Solheim na ujumbe wake .

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameliomba Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) kuisaidia Tanzania kukabiliana na tatizo kubwa la uharibifu wa mazingira katika maeneo mbalimbali nchini ambao umepelekea mamia ya ekari za misitu kutoweka kutokana na ukataji wa miti kwa ajili ya kutengeneza mkaa.


Makamu wa Rais 
Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo wakati alipokutana na kufanya 
mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) Ikulu Jijini Dar es Salaam.


Makamu wa 
Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema pamoja na Serikali kufanya jitihada kubwa 
za kukabiliana na tatizo la uharibifu wa mazingira ikiwemo mpango wa upandaji 
wa miti kote nchini lakini bado msaada na nguvu zaidi inahitajika kutoka 
shirika la Mazingira la UNEP ili kuongeza kasi ya kukabiliana na tatizo hilo 
nchini.


Amesema 
Tanzania ina mahusiano mazuri na ya muda mrefu na Shirika la UNEP ambapo 
shirika hilo limeweza kuisaidia nchi katika miradi mbalimbali ya kuhifadhi 
mazingira hivyo mahusiano hayo mazuri ni muhimu yakaja na mbinu bora na nzuri 
za kuhifadhi mazingira ili kuokoa Taifa lisigeuke jangwa kutokana na uharibifu mkubwa 
wa mazingira unaoendelea nchini.Makamu wa 
Rais pia amehimiza wataalamu wa mazingira wajikite zaidi katika kutoa elimu kwa 
wananchi watumie nishati mbadala kama gesi na makaa ya mawe ili kudhibiti 
tatizo kubwa la uharibifu wa mazingira ikiwemo ukataji wa miti kwa ajili ya kutengeneza 
mkaa.
Kwa upande 
wake, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa ERIC SOLHEIM amepongeza 
jitihada zinazofanywa na Serikali ya kukabiliana na uharibifu wa mazingira na 
kusisitiza kuwa Shirika hilo litaendelea kushirikiana na Serikali Tanzania 
katika Uhifadhi wa mazingira nchini.
Mkurugenzi 
huyo amesema suala la kukabiliana na tatizo la uharibifu wa mazingira sio la Serikali 
pekee hivyo ni muhimu kwa Serikali kushirikiana ipasavyo na mashirika yasiyo ya 
kiserikali katika kupambana na tatizo ili kupata suluhu ya kudumu.
Naye, Waziri 
wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira January Makamba amesema 
ujio wa Mkurugenzi Mkuu wa UNEP hapa nchini ni fursa ya kipekee ya kufungua na 
kuimarisha ukurasa mpya wa mahusiano kati ya Tanzania na UNEP.


Makamba amesema 
kuwa Serikali imetengeneza programu mpya Tano za mazingira ikiwemo kupunguza 
matumizi ya mkaa ili kuhifadhi misitu,vyanzo vya maji,kushughulikia taka na 
kujenga uwezo kama hatua mpya kabisa ya kukabiliana na uharibifu wa mazingira 
nchini.

Related

Hot Stories 6986675393749811397

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item