TPB BANK SASA YAJA KATIKA MUONEKANO NA JINA JIPYA | LUKAZA BLOG

TPB BANK SASA YAJA KATIKA MUONEKANO NA JINA JIPYA

 Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango (kulia) akizindua nembo mpya na jina jipya la iliyokuwa Benki ya Posta Tanzania na sasa i...


 Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango (kulia) akizindua nembo mpya na jina jipya la iliyokuwa Benki ya Posta Tanzania na sasa inajulikana kama TPB Bank Plc, ikiwa ni mabadilko yaliyofanywa baada ya benki hiyo mwaka jana kuorodheshwa chini ya sheria ya makampuni.


Benki hiyo ambayo ina miaka 92 tangu kuanzishwa  kwake, ilibadilishwa uendeshaji wake baada ya mwaka 2015, Bunge kufuta sheria iliyoanzisha benki hiyo na kuifanya kuwa kampuni ili kusajiliwa chini ya Sheria ya Makampuni, mchakato uliokamilika mwishoni mwa mwaka jana na kwa sasa inaitwa TPB Bank Plc.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB Bank, Sabasaba Moshingi akizungumza wakati wa uzinduzi wa jina hilo jipya na nembo ya Benki hiyo Dar es Salaam leo. 


Moshingi 
alisema mabadiliko hayo yanakwenda sanjari na mabadililo makubwa ndani ya benki 
hiyo.“Benki iliamua kubadilisha nembo ili kwenda 
sambamba na jina hilo  na mabadiliko ya 
kuboresha benki ili yanayoendelea,” alisema Moshingi na kuongeza kuwa kwa sasa 
wako katika mchakato wa kujiorodhesha kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam 
(DSE) na kuwa ni fursa ya Watanzania kununua hisa katika benki hiyo ambayo 
faida yake imekuwa ikikua kila wakati.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, TPB Bank, Profesa Lettice Rutashobya akizungumza.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango, akizungumza na kuipongeza TPB Bank kwa hatua iliyofikia na kusema kuwa serikali iko katika mikakati ya kuhakikisha nchi inafikia uchumi wa 
viwanda ifikapo mwaka 2025, na kuwa sekta ya fedha ambayo inakuwa kwa kasi ina 
mchango mkubwa katika kufikia azma hiyo. 
 Alisema serikali ambayo inamiliki benki hiyo kwa 
asilimia kubwa, ingependa kuiona faida ya uwekezaji wake kwa uongozi 
kuhakikisha wanapelekahuduma zao katika kusaidia sekta ya viwanda kwa kutoa mikopo.
 Mmoja wa Maofisa wa TPB Bank akielezea nembo mpya ya benki hiyo na maana yake.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango akimpongeza Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, TPB Bank, Profesa Lettice Rutashobya
 Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango (katikati) akiwa na Afisa Mtendaji wa Tpb Bank, Sabasaba Moshingi na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki hiyo, Prof.Lettice Rutashobya wakifurahia mabadiliko na jina ;la iliyo kuwa benki ya Posta Tanzania ambayo jana Waziri Mpango alizindua jina na nembo mpya.
 Meza kuuu ikifuatilia matukio.
 Wafanyakazi na wageni mbalimbali waalikwa wakifuatilia matukio.
Mgeni rasmi alipewa zawadi ya saa ya Ukutani iliyo na nembo mpya ya TPB Bank.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango akipokea kadi ya TPB popote kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo.
Wafanyakazi wakifuatilia matukio na kusikiliza hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa.
Picha mbalimbali za pamoja pia zilipigwa.

Related

Biashara 6210414596575974456

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item