Wanafunzi SAUT wafanya ziara ya mafunzo TBL Mbeya | LUKAZA BLOG

Wanafunzi SAUT wafanya ziara ya mafunzo TBL Mbeya

Wanafunzi wa SAUT wakiingia katika eneo la kiwanda  b aadhi ya wanafunzi wakiangalia hatua mbalimbali za uzalishaji walipotembelea ki...

Wanafunzi wa SAUT wakiingia katika eneo la kiwanda
 baadhi ya wanafunzi wakiangalia hatua mbalimbali za uzalishaji walipotembelea kiwanda cha TBL Mbeya
Wanafunzi wakipatiwa maelezo ya upimaji wa viwango vya bia katika maabara ya kiwanda kutoka kwa Fundi wa maabara,Sylivester George
Wanafunzi wakipatiwa maelezo ya Usalama wakati wa ziara hiyo
Wanafunzi wakipatiwa maelezo ya taratibu za uzalishaji unavyofanyika kiwandani hapo kutoka kwa Afisa wa TBL,Bw.Joseph Mashila
Meneja wa kiwanda cha TBL Mbeya,Jemedari Waziri ,akiongea na wanafunzi wa SAUT wakati wa ziara hiyo.

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine tawi la Mbeya    wamefanya ziara ya mafunzo katika kiwanda cha TBL cha Mbeya ambapo waliweza kushuhudia kasi ya mabadiliko ya kiteknolojia ya uendeshaji wa viwanda kwa njia ya kisasa unaotekelezwa na kampuni hiyo hapa nchini.

Katika ziara hiyo wanafunzi hao walitembezwa kwenye vitengo mbalimbali vya kiwanda  hicho kinachoongoza kwa ubora barani Afrika na kuongea na wataalamu mbalimbali na kujionea mitambo ya uzalishaji kinywaji cha bia ya kisasa.

Meneja wa kiwanda hicho,Waziri Jemedari , aliwaeleza wanafunzi hao kuwa kiwanda hicho kinaendeshwa na wafanyakazi wazawa na siri ya mafanikio yake ni uwekezaji mkubwa uliofanywa na kampuni kwa kufunga mitambo ya kisasa,kutumia mifumo bora ya uendeshaji wa viwanda ya kimataifa, na kuwa na timu ya wafanyakazi waliobobea katika fani mbalimbali wanaofanya kazi kwa ushirikano mkubwa kwa kujituma.

Jemedari aliwaeleza wanafunzi hao jitihada mbalimbali zinazofanywa ka kampuni katika kuunga mkono jitihada za serikali za kuifanya Tanzania nchi ya viwanda na kufanya uzalishaji usio na athari kwa mazingira.

“Tumeanza kwa kasi kufanya kazi na wananchi katika maeneo tunayofanyia biashara kwa kusaidia miradi mbalimbali yenye mwelekeo wa kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu  kama ulivyo mtizamo wa kampuni na mafanikio makubwa yameanza kupatikana hususani katika  nyanja za uchumi, ustawi wa jamii na utunzaji wa mazingira”.Alisema.
Alisema kampuni imejikita katika kutunza mazingira,kuboresha huduma za maji na uhamasishaji wa matumizi mazuri ya maji,kusaidia wanawake kwenye miradi ya kiuchumi endelevu,kutoa elimu ya ujasiriamali na unywaji kistaarabu,kusaidia wakulima kujikwamua kiuchumi kupitia shughuli za kilimo,kupanua wigo wa ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja na kusaidia miradi katika sekta ya afya na elimu.

Kuhusu mazingira aliwaeleza kuwa kampuni inatekeleza maazimio mbalimbali ya utunzaji mazingira ,kulinda vyanzo vya maji na kupunguza uchafuzi wa hewa kutokana na shughuli za uzalishaji ambapo  tayari imeanza kufanya uzalishaji wa kutumia umeme wa jua katika kiwanda cha Mbeya na uzalishaji wa kutumia pumba za mpunga katika kiwanda cha Mwanza na inaendelea na zoezi la kuingiza teknolojia za kisasa ambazo ni rafiki kwa mazingira.

Aliwaasa wanafunzi hao kusoma kwa bidii na kuwa tayari kupambana na changamoto zilizopo katika soko la ajira na kuwa tayari kutumia elimu waliyoipata kwa vitendo ili kuchangia kuleta maendeleo kwa nchi “Kinachotakiwa ni kujiamini na kufanya kazi kwa bidii ndipo mtaweza kutimiza ndoto zenu na kupata mafanikio”.Alisema.

Related

kitaifa 8915122788058775814

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item