ZAIDI YA WAKULIMA 60,000 KUNUFAIKA NA MRADI WA( AMDT) | LUKAZA BLOG

ZAIDI YA WAKULIMA 60,000 KUNUFAIKA NA MRADI WA( AMDT)

Wakwanza kushoto ni akiyevaa tshirt nyekundu ni Hellen Wakuganda kutoka Asasi ya kusaidia sekta binafsi ya kilimo(PASS)akifuatiwa na aliy...

Wakwanza kushoto ni akiyevaa tshirt nyekundu ni Hellen Wakuganda kutoka Asasi ya kusaidia sekta binafsi ya kilimo(PASS)akifuatiwa na aliyepo katikati Al-Amani Mutarubukwa kutoka (AMDT)akifuatiwa na Juliana Nganyangwa kutoka (AMDT)wakitoa elimu kwa wakulima Jijini Arusha.Picha na Vero Ignatus Blog.27 january 2017.

Na.Vero Ignatus,Arusha. 

Taasisi ya kuendeleza mifumo ya kimasoko katika kilimo Tanzania (AMDT)imewataka wakulima kubadilisha kilimo kuwa biashara ,waondokane na kilimo cha kawaida na kuwa na kilimo cha kisasa na kufahamu kilimo mkataba.

Hayo yamesemwa na meneja mradi Martin Mgallah alipokuwa katika maonyesho ya zana za kilimo Jijini Arusha na kusema kuwa wametenga zaidi ya dola za kimarekani milioni kumi na tano kwaajili ya kuwawezesha wakulima katika zao la Alizeti pekee ndani ya  miaka mitano (2016-2021)

“Taasisi itamuwezesha mkulima kuongeza kipato chake cha mwaka kwa kubadilisha kilimo kuwa biashara,tunaangalia pia mfumo wa masoko,tunamuwezesha mkulima kufahamu kilimo mkataba yaani akishalima na kuvuna mazao yake asihangaike tena kutafuta
soko bali atauza mazao yake kwa bei nzuri,tunamuunganisha na soko moja kwa moja”alisema meneja mradi Martin. 

Amesema kuwa wakulima zaidi ya 60,000 watanufaika na mradi huo,huku akianisha mikoa ambayo wataanza nayo ambayo ni pamoja na Manyara,Shinyanga,Singida,Dodoma,Iringa,Njombe,Mbeya Songwe ,Katavi,Lindi,Rukwa na Mtwara.

Martin amesema kuwa lengo kubwa la( AMDT) kuhakikisha kuwa mkulima anazalisha kilicho bora ,amesema mazao ambayo wataanza nayo ni Alizeti,mahindi,na jamii ya mikundekunde katika mikoa tajwa.Aidha amesema kwaba wanampatia mkulima elimu sahihi,namna ya kulima kilimo cha kisasa,kumuelimisha mkulima  kuwa na bima
itakayomuwezesha kupata nyezo za kisasa za kilimo hivyo amewataka wakulima kuwatembelea ili waone ni kwa namna gani wanaweza kunufaika na program hii.

Related

kitaifa 4172969938833428543

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item