TBL Group yaadhimisha Valentine na wanafunzi wenye ulemavu wa akili | LUKAZA BLOG

TBL Group yaadhimisha Valentine na wanafunzi wenye ulemavu wa akili

  Afisa    uhusiano na mawasiliano wa TBL Group Amanda Walter, (kushoto) akiwakabidhi msaada wa madaftari wanafunzi wenye ulemavu wa kusi...

 Afisa  uhusiano na mawasiliano wa TBL Group Amanda Walter, (kushoto) akiwakabidhi msaada wa madaftari wanafunzi wenye ulemavu wa kusikia wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Msasani jijini Dar es Salaam
 Wafanyakazi wa TBL Group wakicheza na watoto wanaosoma katika shule ya Msasani
 Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Group katika picha ya pamoja na watoto wenye ulemavu wanaosoma katika shule ya msingi Msasani jijini Dar es Salaam
 Baadhi ya wafanyakazi wakigawa zawadi kwa watoto wenye ulemavu wanaosoma katika shule ya msingi y Uhuru Mchanganyiko
Wafanyakazi wa Kiwanda cha Bia TBL Mwanza wakiwapa zawadi wanafunzi wenye ulemavu wa Kituo cha watoto wenye ulemavu Huruma Special Unit

Wafanyakazi wa kampuni ya TBL Group wameitumia siku ya Wapendanao kusaidia na kutoa faraja kwa watoto wanaosoma kwenye shule za walemavu katika mikoa ya Dar es Salaam,Mwanza,Mbeya,Kilimanjaro na Arusha ambapo pia walitoa misaada ya kufanikisha masomo kwa wanafunzi  hao.

 Kwa kutumia kauli mbiu ya Sambaza upendo,Sambaza furaha wameweza kutekeleza moja ya mkakati wa kampuni kuhudumia jamii kukabiliana na changamoto mbalimbali katika maeneo inakofanyia biashara zake ikiwemo kuhamasisha wafanyakazi wake kutumia muda katika shughuli mbalimbali za kijamii.

 Meneja Mawasiliano wa TBL Group,Amanda Walter,amesema kuwa  wameamua kuitumia siku hii kusambaza upendo na furaha kwa watoto wa shule zenye wanafunzi wenye ulemavu ambapo wafanyakazi wamezitembelea na kushiriki shughuli mbalimbali katika maeneo hayo ikiwemo kucheza na kutoa zawadi kwa  watoto kwa ajili ya kuwapatia faraja.

 “Mkakati wetu zaidi katika kusaidia changamoto zilizopo kwenye jamii haulengi kutoa fedha na zawadi bali wafanyakazi kujitoa muda wao kushiriki katika  kazi za jamii kama vile kusafisha mazingira,kufundisha watoto.kupaka rangi majengo ya shule,kupanda miti ,kuwatembelea wagonjwa ,kusafisha maeneo ya hospitali na tumekuwa mstari wa mbele pia kushiriki matembezi mbalimbali ya hisani yenye lengo la kuchangia kuondoa changamoto za kijamii”.Alisema Amanda.

 Alisema TBL Group itaendelea kushiriki shughuli za kijamii kwa kuwa moja ya sera yake ni kuwaleta watu pamoja na kufanya maisha yao kuwa murua inaelekeza kusaidia jamii na kuleta maendeleo endelevu kwa jamii kupitia biashara zake. “Kampuni imekuwa mstari wa mbele kusaidia kukabiliana na changamoto  mbalimbali hususani katika sekta ya elimu,afya na maji ,uwezeshaji wanawake kiuchumi na kampeni za usalama barabarabani.

 Mkurugenzi wa Kituo cha watoto wenye ulemavu Huruma Special Unit, Andrew Jacob ameishukuru kampuni ya TBL Group na wafanyakazi wake kwa kuwakumbuka watoto  wenye mahitaji maalumu hususani katika kuadhimisha siku ya wapendanao,”Kwa niaba ya shule nawashukuru na mmedhihirisha upendo wa kweli kwa kuwakumbuka watoto hawa na kushirikin kucheza nao na kuwapatia zawadi na faraja ya upendo”.Alisema.

Related

Kijamii 3358890970727619801

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item