WATANZANIA 132 WARUDISHWA KUTOKA MSUMBIJI | LUKAZA BLOG

WATANZANIA 132 WARUDISHWA KUTOKA MSUMBIJI

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Dk Suzan Kolimba Idadi ya Watanzania waliofukuzwa Msumbiji imeongezeka mpaka kufikia 132, huku id...

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Dk Suzan Kolimba


Idadi ya Watanzania waliofukuzwa Msumbiji imeongezeka mpaka kufikia 132, huku idadi hiyo ikitarajiwa kuongezeka zaidi kutokana na operesheni ya kuwarudisha nyumbani wahamiaji haramu.

Akizungumzia suala hilo leo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Dk Suzan Kolimba amesema operesheni hiyo haijawalenga Watanzania pekee bali raia wa nchi nyingine walioingia Msumbiji kinyume cha utaratibu.

Dk Kolimba amesema mji wa Montepuez uliopo jimbo la Cabo Delgado una Watanzania 3,000 wanaoishi huko na kwamba idadi ya watakaoondolewa inaweza kuongezeka zaidi.

"Tunaendelea kufuatilia tuhuma za baadhi ya Watanzania kwamba walifanyiwa ukatili wakati wanarudishwa nyumbani ili tujue hatua za kuchukua. Maofisa wetu wanashirikiana na serikali ya Msumbiji katika kuhakikisha Watanzania hawapati matatizo katika operesheni hiyo," amesema.

Related

Hot Stories 3617176381084302634

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item