Airtel yazindua HATUPIMI bando, Ongea bila kikomo | LUKAZA BLOG

Airtel yazindua HATUPIMI bando, Ongea bila kikomo

  Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel, Beatrice Singano Mallya (katikati) akizungumza jijini Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi wa Ofa k...

 Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel, Beatrice Singano Mallya (katikati) akizungumza jijini Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi wa Ofa kabambe ijulikanayo kama Hatupimi Bando itakayowawezesha wateja wake kuongea bila kikomo.  Wa (pili kushoto) ni Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Isack Nchunda na wasanii wa kundi la Weusi, Joe Makini (kulia), Niki wa Pili(wa pili kulia) na Gnako
 Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Isack Nchunda (kushoto)  akizungumza jijini Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi wa Ofa kabambe ijulikanayo kama Hatupimi Bando itakayowawezesha wateja wake kuongea bila kikomo.  Wa (pili kushoto) ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel, Beatrice Singano Mallya na wasanii wa kundi la Weusi, Joe Makini (kulia) na Niki wa Pili.
 Wasanii wa kundi la Weusi, Joe Makini (kulia) ,  Niki wa Pili (katikati) na Gnako wakitumbuiza jijini Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa Ofa kabambe ya Airtel ijulikanayo kama Hatupimi Bando itakayowawezesha wateja Airtel kuongea bila kikomo.
 Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel, Beatrice Singano Mallya (katikati) akisisitiza jambo  wakati wa uzinduzi wa Ofa kabambe ijulikanayo kama Hatupimi Bando itakayowawezesha wateja wake kuongea bila kikomo
 Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel, Beatrice Singano Mallya (wa pili kushoto)  na wasanii wa kundi la Weusi, Joe Makini (kulia), Niki wa Pili(wa pili kulia) na Gnako kwa pamoja  wakizindua Ofa kabambe ijulikanayo kama Hatupimi Bando itakayowawezesha wateja wake kuongea bila kikomo.  Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Isack Nchunda.

·         Airtel yazindua bando la HATUPIMI dakika zenu za muda wa maongezi
·         Wateja wa Airtel kufurahia kuongea bila kikomo kwa siku, wiki na mwenzi
Dar es Salaam, Jumanne 21  Machi 2017, Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel  Tanzania leo imezindua OFA kabambe  ijulikanayo kama HATUPIMI Bando  itakayowawezesha wateja wake wote nchini kuongea bila kikomo mara tu baada ya kujiunga.
“Airtel HATUPIMI Bando” itapatikana katika  vifurushi mbalimbali ikiwemo kifurushi cha  siku, wiki na mwezi  vilivyosheheni  dakika zisiso na kikomo zinazowawezesha wateja wa Airtel kuongea na kufanya mengi zaidi bila kuwa na wasiwasi wa kuishiwa muda wa maongezi kwa kuwa hakuna kupimiwa dakika za maongezi.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa ofa hii kabambe,  Mkurugenzi wa Masoko, Isack Nchunda alisema “ Airtel Hatupimi, sasa Hatupimi dakika zenu za maongezi, tunaleta huduma hizi nafuu kwa kuwa tunaamini katika kuendelea kuboresha huduma zetu  ili kukidhi mahitaji ya wateja wetu kwa  kuwapatia thamani ya pesa zao katika huduma na bidhaa zetu.
“HATUPIMI Bando”  itawapatia wateja wetu nchi nzima uhuru wa kuongea na familia, marafiki na wadau wa biashara zao kulingana na aina ya kifurushi mteja alichochagua ikiwemo kifurushi cha siku, wiki na mwezi bila kujali vifurushi vyao kuisha muda wa maongezi. Kuna vifurushi vya Hatupimi kwa siku vya hadi shilingi 1000/= pia vipo vya wiki kwa shilingi 5000, na vilevile unaweza kujiunga na HATUPIMI kwa mwezi kwa shilingi 10,000/= ili ufurahie huduma yakutopimiwa dakika zako ongea bila kikomo
Airtel tunaamini “HATUPIMI” ni ofa ya kipekee sokoni, tunatoa wito kwa wateja wetu na wateja wapya kujiunga sasa na kufurahia ofa hii kabambe inayowapa uhuru wakuonge watakavyo bila kikomo. Aliongeza Nchunda
Kujiunga na ofa ya HATUPIMI Bando piga *149*99# kisha chagua 1 kupata HATUPIMI kisha chagua bando ya Siku, Wiki, Mwezi kulingana na mahitaji yako “ alisisitiza  Nchunda.
Airtel imekuja  na ofa yake ya HATUPIMI ikiwa ni siku chache tu baada ya kuzindua ofa kabambe kupitia huduma ya Airtel Money, Vile vile airtel wiki hii ilizindua kampeni ya kufungua maduka yake 2,000 yatakayotoa huduma kwa wateja ili kuwafikishia wateja wake wote huduma zao popote walipo.

Related

Hot Stories 953604501199619766

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item