AJALI YA GARI YATOKEA KIMARA SUKA JIJINI DAR ES SALAAM, WAMSHAMBULIA MWANDISHI ALIYEKUWA AKICHUKUA PICHA ZA TUKIO | LUKAZA BLOG

AJALI YA GARI YATOKEA KIMARA SUKA JIJINI DAR ES SALAAM, WAMSHAMBULIA MWANDISHI ALIYEKUWA AKICHUKUA PICHA ZA TUKIO

Gari aina ya Mark II Grand yenye namba za usajili T145AMZ likiwa limeivaa daladala lenye namba za usajili T992DGZ lililokuwa limepaki...

Gari aina ya Mark II Grand yenye namba za usajili T145AMZ likiwa limeivaa daladala lenye namba za usajili T992DGZ lililokuwa limepaki kituoni KIMARA -SUKA jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwa wapo eneo la tukio ilionyesha dereva wa gari hilo dogo alikuwa amelewa na ndipo aliposhindwa kukamata breki na kujikuta uvunguni kwa daladala hilo.
Vijana wakijaribu kuiba katika gari ndogo iliyokuwa imepata ajali eneo la Kimara Suka jijini Dar es Salaam.
Vijana ambao walivamia gari ndogo na kuanza kuiba wakishangaa kuona kamera ya Kajunason Blog imetinga eneo hilo na ndipo walipoungana na mwenye gari kumfanyia fujo na kumpiga kwa kumshambulia mwandishi wa habari Cathbert Angelo Kajuna aliyekuwa eneo la tukio. Kwa msaada wa wasamalia wema waliweza kumnasua mwandishi huyo na kuweza kumshika kijana aliyekuwa mmiliki wa gari ndogo ambaye ndiye alitoa amri ya kumshambulia mwandishi wa habari.

Kijana aliyemshambulia mwandishi wa habari Cathbert Angelo Kajuna amekatwa na kufunguliwa jarada la KMR/RB/3987/2017 na mpaka sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kituo cha Mbezi kwa Yusuph.

Related

kitaifa 2860398181969859769

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item