Flash News: MBUNGE TUNDU LISSU AKAMATWA NA POLISI AKITOKA MAHAKAMANI | LUKAZA BLOG

Flash News: MBUNGE TUNDU LISSU AKAMATWA NA POLISI AKITOKA MAHAKAMANI

Jeshi la Polisi nchini linamshikilia Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu baada ya kuachiwa huru na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu...

Jeshi la Polisi nchini linamshikilia Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu baada ya kuachiwa huru na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Lissu aliachiwa leo asubuhi na Hakimu Mkuu Mkazi, Huruma Shahidi baada ya upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili Paul Kadushi kuwasilisha hati ya kuondoa shtaka hilo.

Kadushi aliwasilisha hati hiyo chini ya kifungua namba91 (1) cha makosa ya jinai akionyesha DPP hana haja ya kuendelea na kesi, mahakama ikaridhia na kumuachia.

Muda mfupi baada ya kuachiwa na kutoka nje ya mahakama alikamatwa tena na askari waliokuwapo mahakamani hapo na kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi.

Lissu alikuwa anashtakiwa kwamba Januari 11, mwaka huu katika kampeni za uchaguzi jimbo la Dimani aliwashawishi watu wasiridhike na wawe na nia ovu dhidi ya utawala.

Related

Hot Stories 8220023009378533123

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item