Hukumu kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na Jamii Media yatoka na hii ndio hukumu yenyewe | LUKAZA BLOG

Hukumu kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na Jamii Media yatoka na hii ndio hukumu yenyewe

Mahakama Kuu imesema Vifungu vya Sheria vilivyopingwa na Jamii Media, vipo sawa kikatiba ila imekiri sheria kutumiwa bila kanuni ni ch...Mahakama Kuu imesema Vifungu vya Sheria vilivyopingwa na Jamii Media, vipo sawa kikatiba ila imekiri sheria kutumiwa bila kanuni ni changamoto. Pamoja na kusema vifungu vipo sawa, imezitupilia mbali hoja zote za Serikali
⁠⁠⁠⁠
⁠⁠⁠Hoja za Upande wa Jamii Media zilikuwa ni:

1) Sheria inaendeshwa bila kanuni, hivyo inavunja haki za binadamu

2) Vifungu vya 32 na 38 vinatumika visivyo; hivyo vitangazwe kuwa kinyume cha Katiba

⁠⁠⁠⁠Mahakama Kuu yatoa mwongozo wa kesi yoyote chini ya kifungu cha 32 ya Sheria ya Mitandao, polisi lazima waende mahakamani kuomba mahakama ishurutishe mtoa huduma kutoa taarifa.
⁠⁠⁠⁠
⁠⁠⁠Mwanasheria Ben Ishabakaki kaeleza kuwa tafsiri ya kauli hii ya Mahakama Kuu kisheria ina maana kesi za jinai zilizofunguliwa dhidi ya #FreeMaxenceMelo hazijafuata sheria kwa sababu polisi walitakiwa waende kwanza mahakamani badala la kukamata na kufungua mashtaka moja kwa moja.

Wamesema kifungu kipo kinachowataka Polisi kwenda mahakamani endapo watanyimwa data kabla ya hatua wanazochukua dhidi ya Jamii Media kama mtoa huduma.
⁠⁠⁠⁠
⁠⁠⁠Mahakama Kuu yamwonya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kutohoji Mamlaka ya Mahakama katika kutafsiri sheria.
⁠⁠⁠⁠
⁠⁠⁠Mahakama yasisitiza kuwa sheria zilizopo zinahitaji kuzingatia maendeleo ya teknolojia na Haki ya Faragha

Mahakama imeongeza kuwa kuna umuhimu wa kuwa na Kanuni za kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Makosa ya Mitandao
⁠⁠⁠⁠
⁠⁠⁠"Ni muhimu kujua nani wako nyuma ya msukumo huu wa kupata data za watumiaji. Hatupambani na Dola" - Maxence Melo

Related

Hot Stories 2780966284949102791

Post a Comment Default Comments

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

emo-but-icon

SEDUCE ME BY ALI KIBA

TMT 2016.FILAMU NDIO SISI

Winner ABA 2015

BOOK ME - YOUR JOB NEEDS ME

All Recent Posts

>

Connect Us

item